Airtel yashiriki uwekaji wa Mkongo wa mawasiliano kutoka Dar-Tanzania hadi nchini Shelisheli

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya (kushoto) na Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando wakijibu maswali ya wanahabari wakati wa uzinduzi rasmi wa uwekaji wa mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar es Salaam Tanzania hadi nchini Seychelles katika eneo la Msasani, jijini humo jana.  Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia mradi huo.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya ( wa nne kushoto) akisaidia kazi ya uwekaji  wa mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar es Salaam Tanzania hadi nchini Seychelles katika eneo la Msasani, jijini humo jana katika hafla ya uzinduzi rasmi wa uwekaji huo ambao  Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia utekelezaji wake. Wengine ni mafundi na wawakilishi wa makampuni yanayosimamia mradi huo.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Waziri wa Maliasili na Viwanda wa Shelisheli Bw. Peter Sinon amesema nchi yake itanufaika na upatikanaji wa mawasiliano ya mkongo wa taifa kutoka Tanzania kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya taifa hilo.
Mkongo wa taifa wa mawasiliano uliozinduliwa miaka 2 iliyopita na Rais Jakaya Kikwete umeweza kuzinufaisha nchi jirani kama Kenya, Uganda, Rwanda,Burundi na sasa Shelisheli.

Akiongea katika fukwe za bahari ya hindi jijini Dar es Salaam eneo la msasani ambako uwekaji wa mlongo huo ndio ulikoanzia mwishoni mwa wiki hii Waziri Sinon amesema kuwa mpango huo ukimalika utaiweza nchi yake kukuza sekta ya mawasiliano na upatikanaji wa taarifa mbalimbali jambo litakalo saidia kukuza uchumi wa nchi hiyo.

“Hii ni nafasi nzuri ya kipekee na ndio maana hata sisi shelisheli tunaipa kipaumbele ili kukamilisha zoezi hili la uwekaji wa mkongo huu wa mawasiliano, tunaamini tukimaliza kila kitu itasaidia sana kukuza pato la nchi kulingana na umuhimu wa mawasiliano” alisema Bw Peter Sinon- Waziri wa Maliasili na Viwanda Shelisheli
 
Kwa uapnde wake Katibu Mkuu Kiongozi kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais wan chi hiyo anayeshughulikia ICT, Bw Benjamin Choppy ameelezea faida za uwepo wa mkongo huo kuwa ni pamoja na kutoa mawasiliano ya uhakika na bora kwa nchi hiyo

“Sasa hii ni dalili ya kutoa bidhaa bora ya mawasiliano kwa kuwa ukamilifu wa uwekaji mkongo huu tutapata mwasiliano bora zaidi” alimaliza kwa kusema Katibu Mkuu kiongozi kwenye ofisi ya makamu wa rais wan chi hiyo anayeshughulikia ICT Bw Benjamin Choppy.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano Mallya ameelezea upatikanaji wa teknolojia hiyo mpya ya mawasiliano kuwa ni kati ya vitu ambavyo Airtel inavifanyia kazi kuhakikisha inaunganisha mataifa mengi ili kutoa mawasiliano yanayotoa nafasi au fulsa ya kuendeleza nchi hizo kijamii na kiuchumi pia.
 
“tunaamini ushirikiano wetu na wenzetu wa shelisheli ni dhahiri utachangia sana kuboresha mahusiano yetu kibiashara na pia kutoa nafasi kwa nchi hizi kujijenga kijamii ma kiuchumu kutokana na faida ya mahusiano haya ya kulaza mkongo huu wa kuunganisha mawasiliano” alisema Bi Beatrice Singano Mallya.

Aitel Tanzania na Airtel Shelisheli kwa kushirikiana na SCS zinatekeleza mpango wa kuweka mkongo wa taifa kwa lengo la kuiwezesha nchi hiyo kuwa na mawasiliano ya uhakika.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI