Hivi ndivyo Fusu hilo lilivyokuwa baada ya ajali
  Wananchi na polisi wakisaidiana kuinasua miili ya watu watatu walio kufa katika ajali
 Mwili wa dereva Taxi ukiwa bado kutolewa
 Wananchi na polisi wakisaidiana kuinasua miili ya watu watatu walio kufa katika ajali
 Wananchi wakitazama Fuso ambalo liligongana na Taxi hiyo
 skari wa usalama barabarani mjini Iringa wakiwa wamebeba moja kati ya maiti za ajali ya Taxi na Fuso iliyotokea eneo la kituo cha Mafuta Eso kwenye barabara kuu ya Iringa -Mbeya asubuhi hii
 Miili ya wafanyakazi wa barabara Iringa ambao walikufa katika ajali hiyo
Ajali mbaya imetokea mjini Iringa asubuhi hii na kusababisha vifo vya watu watatu papo hapo huku abiria waliokuwemo katika fuso wakinusurika katika ajali hiyo .Mashuhuda waliozungumza na Mdau  Francis Godwin wamedai kuwa Taxi hiyo yenye namba za usajili T620 ANE ilikuwa ikitokea Ndiuka ikiwapeleka wafanyakazi wa barabara katika eneo la Tanangozi am,bako ujenzi wa barabara kuu ya Iringa -Mbeya uinaendelea .

Hata hivyo kabla ya kufika katika eneo hilo la kituo0 cha Mafuta cha Eso dereva wa Taxi hiyo ambaye alikuwa akitaka kulipita gari jingine lililokuwa mbele yake alishindwa kulipita gari hilo baada ya kukutana uso kwa uso la Fuso yenye namba za usajili T897 AQS ambalo lilikuwa limeshehena magunia ya mpunga .

Hivyo kutokana na mwendo kasi ambao Fuso hilo lilikuwa likienda nao na mwendo kasi wa Taxi hiyo uwezekano wa kukwepana ulishindikana na hivyo kupelekea fuso hilo kuigonga Taxi hilo na kuipitia kwa juu na kupelekea vifo vya abiria wawili na dereva wa Taxi hiyo papo hapo .

Jitihada za kuzitoa maiti hizo zinaendelea hadi sasa japo eneo la tukio likiwa limetapakaa ubongo wa maiti hizo za ajali na wasamaria wema wakiendelea kufanya kazi hiyo ya kuzitoa maiti bila ya kutumia kinga yeyote na hivyo idadi kubwa ya wasamaria wema hao waqmeonekana wakiwa wametapakaa damu. Chanzo;Haki Ngowi Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*