akamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Aongoza Ujembe wa Zanzibar katika Mazungumzo na Waziri wa Biashara wa Cuba

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Waziri wa Biashara za Kigeni na Uwekezaji  wa Cuba Bwana Rodrigo Malmierca Dias, Mjini Havana Nchini Cuba wakati wa ziara yake ya Kiserikali Nchini, humo kushoto kwa       Makamu wa Pili wa Rais ni Balozi wa Tanzania Nchini Cuba Mh. Paul James Makelele.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiongoza Ujumbe wa Zanzibar katika Kikao cha pamoja na Ujumbe wa Wizara ya Biashara za  Nje na Uwekezaji wa Cuba ulioongozwa na Waziri wake Bwana Rodrigo Malmierca Diaz.Picha na Othman Khamis-Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
---     
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema upo umuhimu mkubwa wa kuongeza ushirikiano zaidi kati ya Zanzibar na Jamuhuri ya Cuba hasa katika Sekta ya Biashara na Uwekezaji kwa nia ya kustawisha Uchumi wa Pande hizo mbili.

Balozi Seif alitoa wazo hilo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Biashara za Nje na Uwekezaji vitega uchumi wa Jamuhuri ya Cuba Bwana Rodrigo Malmierca Diaz yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo yaliyopo Mjini Havana Nchini Cuba.

Alisema Maendeleo makubwa na ya haraka yanaweza kupatikana katika kipindi kifupi iwapo pande hizo mbili zitafikia maamuzi ya pamoja katika kuzishirikisha Sekta binafsi kwenye Mpango huo muhimu wa Uchumi.

 Alisema Tanzania na Zanzibar kwa ujumla tayari zimeshafungua milango kwa Taasisi Binafsi za Biashara na Uwekezaji kutoka Nje ya Nchi na kupelekea hali ya Uchumi kukua hatua kwa hatua.

Balozi Seif aliishauri Cuba kuitumia fursa hiyo kwa kuzishawishi Taasisi na Makampuni ya Nchi hiyo kuwekeza Tanzania na Zanzibar kwa Ujumla kwa vile maeneo mengi bado yana rasilimali za kutosha katika uwekezaji Vitega Uchumi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameelezea kuvutiwa kwake na Mfumo wa Utalii unaoendelezwa Nchini Cuba ambao umepelekea Nchi hiyo kukusanya Mapato mengi yatokanayo na Sekta hiyo. “ Zipo baadhi ya changamoto ambazo tumeweza kuzishuhudia katika ziara yetu tuliyoifanya kwenye sekta tofauti ambazo zinakukabilini.

Lakini hili linaweza kupatiwa ufumbuzi wa haraka kwa kutumia njia ya ushirikiano katika kutatuza changamoto hizo”. Alisisitiza Balozi Seif Ali Iddi katika maelezo yake kwa Ujumbe huo wa Wafnyabiashara wa Cuba.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alishauri kuwepo kwa kiunganisho cha mawasiliano kati ya Mji wa Zanzibar, Dar es salaam na Havana katika kuona Sekta ya Biashara inaleta faida kwa pande hizo mbili.

 Akizungumzia Kilimo Balozi Seif alisema Zanzibar iko katika juhudi za kuimarisha ukulima wa Umwagiliaji, hivyo Cuba inaweza kusaidia sekta hiyo kwa vile Tayari imeshakuwa na Wahandisi na wataalamu wa kutosha katika maeneo hayo muhimu.

Naye Waziri wa Biashara za Nje na Uwekezaji Vitega Uchumi Nchini Cuba Bwana Rodrigo Malmierca Diaz alisema Nchi hiyo itaendelea kuwapatia Elimu Watanzania katika ule utaratibu wake inaoutumia wa muda mrefu katika kusaidia Mataifa ya Bara la Afrika.

Bwana Rodrigo alisema Uongozi wa Wizara yake unakusudia kutayarisha mpango Maalum wa kutafuta Taasisi zitakazosaidia Miradi itakayoanzishwa ambapo alilitolea mfano Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni { UNESCO } ambalo tayari limeshazisaidia Nchi za Cuba na Venezuela katika Miradi ya pamoja.

Aliishauri Zanzibar na Tanzania kwa jumla kujiandaa kushiriki katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara yanayotarajiwa kufanyika Nchini humo tarehe 4 hadi 10 Novemba Mwaka huu ili kujijengea uwezo zaidi wa uzalishaji.

 Alisema mualiko rasmi kwa Tanzania wa Ushiriki wa Maonyesho hayo utatolewa hapo baadaye ambapo aliomba fursa hiyo kutumiwa vyema. Cuba kutokana na kuwa na vivutio vingi vya kimaumbile imekuwa ikipokea watalii zaidi ya Milioni mbili kwa mwaka kutoka sehemu mbali mbali Ulimwenguni.
Na
Othman Khamis Ame 
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 
17/5/2012.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*