ANGETILE OSIAH ANG'ATUKA YANGA SC


KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Angetile Osiah ametangaza kujivua nafasi yake ya ujumbe wa kamati ya uchaguzi ya klabu ya soka ya Yanga.
 Osiah amesema kuwa  analazimika kufanya hivyo kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za shirikisho hilo na atawasilisha barua kwa katibu mkuu wa Yanga, Mwesiga Selestine. 
 
Alisema kuwa licha ya kuteuliwa muda mrefu kushika wadhifa wa ukatibu wa TFF, alishindwa kuwasilisha barua ya kujitoa katika kamati ya uchaguzi kutokana na kuingwa na majukumu ndani ya shirikisho hilo. 
 
“Nimelazimika kufanya hivyo kwani kwa sasa Yanga inahitaji kufanya uchaguzi mdogo kwa lengo la kuziba nafasi zilizoachwa wazi na baadhi ya viongozi walioachia ngazi Yanga hivyo inabidi nafasi yangu ijazwe ili kamati iweze kuendesha mchakato wake kikamilifu,”alisema. 
 
TFF kupitia kamati ya uchahizi iliyo chini ya mwenyekiti wake Deogratius Lyato iliiagiza kamati ya uchaguzi ya Yanga chini ya mwenyekiti wake Jaji John Mkwawa ifanye uchaguzi wake kuziba nafasi za nane za viongozi waliojiuzulu na mjumbe mmoja aliyefariki dunia. 
 
Hatua hiyo inafuati hivi karibuni kujiuzulu kwa mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga kutokana na shinikizo la baadhi ya wanachama wakiongozwa na baraza la Wazee waliomtaka kufanya hivyo kwa madai ya kutoiletea mafanikio klabu na hatimaye kupokwa ubingwa wao wa ligi kuu bara ulioenda kwa Simba na wao kuishia nafasi ya tatu. 
 
Awali makamu mwenyekiti wa Yanga Davis Mosha alitangaza kujiengua katika uongozi miezi michache baada ya kuchaguliwa kwa madai ya kutoelewana na Nchunga, huku mjumbe wa kamati ya utendaji, Theonest Rutashoborwa alifariki dunia. 
 
Kama hiyo haitoshi, wajumbe wengine walioachia ngazi Yanga ni pamoja na Seif Ahmed, Mbaraka Igangula, Mzee Yusuf, Ally Mayay, Charles Mgondo  na Mohammed Bhinda. Chanzo; Mama Pipiro blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*