Brotherhood aahidi kujumuisha wote,Misri

Mgombea wa Urais mrengo wa Muslim Brotherhood nchini Misri Mohammed Mursi (pichani), amesema kwamba atajumuisha makundi yote ya kisiasa katika serikali endapo atashinda duru ya pili ya Urais.

Mursi (pichani)ameahidi haya katika mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema atahakikisha kuwepo kwa uwakilishi wa wanawake na vijana.Kiongozi huyo wa chama cha Freedom and Justice amesema kwamba nia yake ni kuondoa utawala wa kiimla na kuweka msingi thabiti katika taasisi za uwongozi.

Matamshi ya Bw. Mursi yanajiri wakati afisi za hasimu wake Ahmed Shafiq zimeteketezwa na watu wanaodhaniwa wafuasi wafuasi wa makundi ya kiisilamu.

Watu wanne wamekamatwa kwa kuhusishwa na tukio hilo.Awali maelfu ya raia waliandamana nje ya makao makuu ya tume ya uchaguzi kufuatia matokeo ya raundi ya kwanza ambapo Bw Mursi alishinda kwa asilimia 24.3 dhidi ya Bw Shafiq aliyepata asili mia 23.3 ya kura.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI