CHELSEA MABINGWA KOMBE LA ULAYA

Drogba

Timu ya Chelsea imeibuka kidedea kwa kufanikiwa kilitwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, kwa kuifunga Bayern Munich kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120, kwenye Uwanja wa Allianz Arena, Munich, Ujerumani.

      Ni Didier Yves Drogba ambaye pamoja na kufunga penalti ya mwisho ya ubingwa, pia alifunga bao la Chelsea ndani ya dakika 90. Lakini pia, sifa zimuendee kipa Petr Cech aliyecheza penalti mbili za Bayern.

     Wengine waliofunga penalty za Chelsea ni David Luiz, Frank Lampard na Ashley Cole, wakati Juan Mata yake iliokolewa Neur.   Kwa upande wa Bayern, waliofunga ni Lahm, Gomez na kipa Neur.

       Katika mtanange huo hadi mapumziko hakuna timu iliyokuwa imefanikiwa kuona lango la mwenzake, Bayern wakitawala zaidi mchezo na kupata kona kibao, lakini safu ya ulinzi ya Chelsea iliyoongozwa na David Luiz ilikuwa imara kuwadhibiti The Bavarians.

     Kipindi cha pili Chelsea nao waliamua kuongeza kasi ya mashambulizi na kupata kona tatu, lakini walikuwa ni Bayern Munich waliotangulia kuwainua vitini mashabiki wao, dakika ya 83 kwa bao la Thomas Mueller, aliyeunganisha kwa kichwa cha kudundisha chini krosi ya Toni Kroos na mlinda mlango wa The Blues, Petr Cech akashindwa kuokoa.

Mara tu baada ya bao hilo, Kocha wa Muda wa Chelsea, Roberto Di Matteo, alimuinua mshambuliaji Fernando Torres kwenda kuchukua nafasi ya Solomon Kalou, jambo ambalo liliongeza uhai wa safu ya ushambuliaji ya Blues.

Alikuwa ni mshambuliaji ambaye anacheza mechi yake ya mwisho na jezi ya Chelsea, Didier Yves Drogba aliyeisawazishia bao timu yake dakika ya 88, kwa kichwa kikali akiunganisha kona iliyochongwa na Juan Mata.

Bao hilo liliwanyamazisha malefu ya mashabiki wa Bavarians walioamini Mueller kamaliza kazi na Kombe linabaki Munich- na tangu hapo timu hizo zilishambuliana kwa zamu hadi kipyenga cha kuhitimisha dakika 90 na mchezo kuhamia kwenye dakika 30 za nyogeza.

Katika dakika ya tatu ya muda wa nyongeza, Drogba alimkwatua kwa nyuma kwenye eneo la hatari Frank Ribery na refa akawapa penalti Bayern sambamba na kumpa kadi ya njano mshambuliaji wa Ivory Coast.

Arjen Robben alikwenda kupiga penalti dakika ya 94 na kipa Petr Cech aliyesema mapema amekwishasoma hatua za wachezaji wa Bayern wakati wa upigani wa penalti, alidhihirisha hilo kwa kupangua mkwaju wa winga huyo wa kimataifa wa Uholanzi.

      Cech ambaye kesho anasherehekea miaka 30 ya kuzaliwa kwake, hakupangilia mbali mpira huo, ilikuwa jirani mno na yeye na akaugeukia haraka na kuuficha kwenye himaya yake.

      Baada ya hapo, timu hizo zilishambuliana kwa zamu na kwa tahadhari mno na hadi dakika 15 za kwanza zinamalizika ubao wa matokeo ulibaki kusomeka 1-1.

     Dakika ya 107, Daniel Van Buyten alipata nafasi nzuri akiwa anatazamana na kipa Cech, lakini shuti lake la chini lilikwenda nje sentimita chache upande wa kuliwa wa kipa huyo wa Chelsea. Huna sababu ya kutosema lilikuwa bao la wazi walikosa Bayern.

      Dakika ya 111 tena Bayern walifanya shambulizi kali langoni mwa Chelsea, lakini Luiz akaokoa na kuna iliyokwenda kupigwa na Robben, lakini ikaondoshwa kwenye hatari.

       Dakika 120 zinatimu matokeo 1-1 na katika matuta, Chelsea wakafuta machungu ya 2008 walipofungwa na Manchester United kwenye fainali mijni Moscow:

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA