Diwani Mathew apata milioni 70 za kuchimba visima, Vijibweni

Diwani wa Kata ya Vijibweni, Kigamboni jijini Dar es Salaam, Suleiman Mathew (kulia), akizungumza na wananchi wa kata hiyo juzi, katika mkutano wa kuwashukuru kwa kumchagua katika nafasi hiyo. (Picha na Dotto Mwaibale)



Vijibweni yapata sh. milioni 70 za kuchimba visima
Na Dotto Mwaibale

SHILINGI milioni 70 zimepatikana Kata ya Vijibweni Kigamboni, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchimba visima virefu ili kukabiliana na tatizo la maji kwa wananchi wa eneo hilo.

Hayo yalibainishwa na Diwani wa Kata hiyo, Suleiman Mathew (CCM), katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mwakilishi wao uliofanyika Dar es Salaam jana.

Alisema fedha hizo zimepatikana kupitia mfadhili ambaye hakupenda kumtaja jina lake na kuwa kila tawi la kata hiyo litanufaika kwa kupata visima viwili.

Alisema mfadhili huyo amesaidia kufadhili uchimbaji wa visima 7 ambapo kila kimoja kitagharimu sh.milioni 10 na kuwa hivi sasa unafanyika mchakato wa kujua mahali pa kuvichimba.

"Tumepata ufadhili mwingine kutoka Kampuni ya Home Shoping Centre (HSC), ambao watatusaidia kuchimba visima vitano na hii itasaidia kuwapunguzia wananchi wangu tatizo hilo la maji lililokuwa likiwakabili kwa muda mrefu" alisema Mathew.

Akiongelea kuhusu mikpo kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika kata hiyo alisema sh. milioni 15 zipo kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wajasiriamali mbalimbali wa eneo hilo.

"Tumetenga sh.milioni 15 kwa ajili ya wajasiriamali wadogo kama wale wanauuza mboga mboga, maandazi, mama lishe na biashara ndogo ndogo ambapo kila mmoja atakopeshwa sh.50,000" alisema Diwani huyo.

Alisema fedha hiyo imepatikana kupitia mfuko wa diwani kwa ajili ya shughuli za maendeleo ambapo mama lishe 200 watanufaika na mkopo huo.

Aliongeza kuwa unafanyika utaratibu wa kutoa semina kwa wajasiriamali hao ili kubaini wale wanaofanya shughuli hizo badala ya mkopo huo kuingiliwa na watu wasiostahili.

Akielezea mpango wa elimu katika hiyo alisema shule nyingi zinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za kukosekana kwa madawati pamoja na uchakavu wa majengo.

"Kutokana na kukabiliana na changamoto za elimu katika kata yetu tumefanikiwa kupata mifuko 400 ya saruji kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa majengo ya shule mbalimbali" alisema Mathew.

Diwani wa Kata hiyo Suleiman Mathew alitumia fursa ya mkutano huo alioutisha kuwashukuru wananchi hao kwa kumchagua na kuwataka kushirikiana kwa kila jambo bila kujali itikadi za vyama ili kuiletea maendeleo kata hiyo na taifa kwa ujumla.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI