GRAND MALT CHAZINDUA TUZO ZA 'EXEL WITH GRAND MALT' KWA WANAFUNZI


Meneja wa kinywaji cha Grand Malt, Consolata Adam (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, kuhusu promosheni ya kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi kuzindua tuzo za 'Exel with Grand Malt"  kwa wanafunzi wa elimu ya juu ikiwa ni mara ya pili kwa tuzo hizo kutolewa ambapo jumla ya sh. milioni 500 zimetengwa kuwazawadia watakaoshinda.  Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butalla
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah (katikati kulia) akifafanua jambo wakati wamkkutano huo
Wanahabari wakiwa kazini
Butallah (katikati), Meneja Uhusiano Mambo ya Nje, Emma Oriyo (kushoto) na Mama Adam wakifurahia jambo baada ya mkutano na wanahabari kumalizika

Kinywaji maarufu cha Grand Malt leo kimezindua tuzo kwa wanafunzi wa elimu ya juu zijulikanazo kama “Excel with Grand Malt”, huu ukiwa ni mwaka wa pili kwa tuzo hizi kutolewa.

Akizungumzia tuzo hizo, meneja wa kinywaji cha Grand Malt Bi. Consolata Adam alisema; Excel with Grand Malt ni tuzo za aina yake ambazo zimelenga kutambua na kuthamini mchango wanaoonesha wanafunzi katika fani mbalimbali nje ya masomo ya darasani. Tunatambua kuwa kazi kubwa ya mwanafunzi anapokuwa chuoni ni kuhudhuria vipindi vya darasani na kupata elimu, bali tunapenda pia kuwatambua wale wachache ambao wanakwenda mbali zaidi na kufanya mambo ya maendeleo katika mazingira yao ya chuo.

Tuzo hizi zilianzishwa mwaka jana ambapo tuliweza kufika katika mikoa sita na kufikia vyuo vipatavyo ishirini. Kwa mwaka huu mchakato utaanza mwezi Aprili hadi June, na Mikoa itakayohusika ni pamoja na Dar es salaam, Morogoro, Iringa, Dodoma, Kilimanjaro na Mwanza ambapo vyuo vipatavyo 21 vitashiriki. Kama ilivyokuwa mwaka jana, fani zitakazoshindanishwa ni Ubunifu (Innovation), Michezo (sports), Utamaduni na burudani (Culture & Entertainment) na Mazingira na Huduma za jamii (Environment & social responsibilities). Kama ilivyo ada, washindi katika fani hizi watajipatia zawadi mbalimbali toka Grand Malt ikiwa ni pamoja na pesa za kununulia vitabu na vyeti vya ushindi.

Kwa sasa natangaza rasmi kuwa tunzo hizi zimezinduliwa rasmi na mkoa wa kwanza utakuwa ni Morogoro ambapo tunatarajia kufanya tamasha kubwa kwenye viwanja vya chuo kikuu cha SUA siku ya jumamosi kisha jumapili tutafanya tamasha la ufunguzi kwenye Viwanja vya chuo cha CBE mkoani Dodoma na kutakuwa na burudani zitakazoongozwa na nguli wa Hip hop nchini Joh Makini ,zawadi nyingi na zaidi kutakuwa na GrandMalt baridi na hakutakuwa na kiingilio chochote. Alisema Bi. Consolata.

Akielezea umuhimu wa Tuzo hizo, meneja masoko wa TBL Bw. Fimbo Butallah alisema; Tunafurahi sana kuona vyuo vyote vilipokea tuzo hizi kwa furaha kubwa, hii ni kwa sababu wanatambua umuhimu wake. Kupitia tuzo hizi ambazo zitakuwa zikitolewa kila mwaka, Grand Malt inatoa changamoto kwa vijana walio vyuoni kuona umuhimu wa kujituma na kufanya mambo mengi na makubwa zaidi ya kufaulu mitihani ya darasani tu. 
Tunaomba viongozi wa serikali za wanafunzi na viongozi wa vyuo kuendelea kutoa ushirikiano kama walivyofanya mwaka jana ili kuleta ufanisi zaidi katika tuzo za mwaka huu. Kama ilivyo kawaida, utaratibu utakuwa ule ule ambapo wanchuo watapendekeza majina ya vijana wanaoamini kuwa wamefanya mambo makubwa ndani ya vyuo vyao katika tasnia zilizotajwa hapo awali, kisha kufuatiwa na kipindi cha kupiga kura ambapo washindi watapatikana. Alimaliza Bw. Butallah

Kwa upande wake meneja mahusiano na mawasiliano wa TBL, Bi. Edith Mushi alisema GrandMalt kwa kuzingatia umuhimu wa juhudi za serikali katika kuhamasisha jamii kutunza mazingira kwa kupanda miti mwaka huu Grand Malt itafanya zoezi maalum kwenye kila chuo kwa kupanda miti imara itakayosaidia kutunza na kuboresha mazingira ya vyuo hivyo ili kuandaa mazingira bora ya kusomea ya wanafunzi wa sasa na wa vizazi vijavyo ambapo mkoani Dodoma zoezi hilo litafanyika jumatatu May 07,2012 katika vyuo vya UDOM na CBE tawi la Dodoma na Mkoani Morogoro zoezi hilo litafanyika kwenye vyuo vya SUA na Mzumbe siku ya jumanne May 08,2012 asubuhi, kisho zoezi hilo litaendelea katika mikoa ya Iringa,kilimanjaro,Mwanza na Dar Es Salaam.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*