H BABA AFUNIKA BONANZA LA TIGO SAME

 Wananchi mkoani Kilimanjaro wakifuatilia kwa karibu Bonanza la Tigo.


 H Baba akitumbuiza na mmoja wa wanafunzi waliokongwa nyoyo na kuamua kupanda jukwaani.

H baba akitumbuiza huku wananchi wakimfuatilia kwa karibu

H Baba akitumbuiza na mmoja wa wananchi waliofika katika Bnanza hilo.

Na Joyce Anael,
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tigo imeendesha Bonanza la aina yake katika viwanja vya Kwasakwasa wilayani Same mkoani Kilimanjaro na kuhudhuriwa na wananchi wengi hususani  wanaotumia mtandao huo lengo likiwa ni kushirikishana mambo mbalimbali yahusuyo mtandao huo.

Akizindua Bonanza hilo Mratibu wa Promosheni kutoka katika kampuni hiyo,Edwin Shilla  alisema lengo la bonanza hilo pamoja na kushirikishana mambo mbalimbali ya tigo pia wamelenga kutoa huduma karibu na jamii.

Shila alisema amefurahishwa sana na watu wa mkoa wa Kilimanjaro ambao walijitokeza kwa wingi katika Bonanza hilo ili kuweza kufurahia pamoja na kampuni hiyo na kupata huduma mbalimbali za mtandao huo.
Aidha aliwataka wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro na nchini kote kuendelea kutumia mtandao wa tigo ambao ni nafuu hapa nchini na unawafika wananchi wote kwa urahisi bila usumbufu.

Akizungumza Ofisa wa Tigo mkoani Kilimanjaro Mohamerd Rajab  Bonanza hili lililenga kuwasogeza kampuni hiyo pamoja na jamii  na kwamba pamoja na maandalizi waliyoyafanya hawakutegemea uwepo wa watu wengi kama walivyojitokeza.

“Kwakweli Tigo ni mtandao wa watu kwani hatukutegemea umati mkubwa wa watu namna hii,hasa katika wakati huu ambao kuna hali ya Mvua,tunawapongeza sana wakazi wa Kilimanjaro hususani wa Maeneo ya Same na Rombo kwa kujitokezza kuja kushuhudia bonanza hili,tumefarijika sana”alisema.

Katika Bonanza hilo ambalo kulitolewa zawadi mbalimbali kama Tishart,Muda wa Maongezi wa Buren a Lain za Tigo,pia  lilipambwa na wanamuziki mbalimbali wa Kizazi Kipya akiwemo H Baba  ambaye alizikonga nyoyo za wanakilimanjaro huku wengi wao wakionekaa kugombania Tishart ya Tigo aliyokuwa amevaa na Namba yake ya Simu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*