Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) yatembelea Waathirika wa Mabomu Mbagala

Mwenyekiti  wa Kamati  ya Bunge ya Hesabu za Serikali  (PAC) John Cheyo (Mwenyekoti) na Katibu wa Kamati ya  (PAC), Ramadhan  Issa  Abdallah (kushoto) pamoja na baadhi ya wanakamati  na watendaji wa Mkoa wa DSM wakiangalia orodha yenye majina  ya  malipo kwa waatihirika wa mabomu ya Mbagala Kuu  walipotembelea Mei 22.2012 huko Mbagala Kuu  na kuangalia maeneo ya wakazi  hao ambayo mengine  yamekarabatiwa. Mwenyekiti  huyo amewashauri  baadhi ya waathirika  hao kwenda  kuchukua hundi  zao haraka  kabla ya zoezi  la malipo kufungwa. Tukio la kulipuka kwa mabomu  lilitokea mwaka 2009 huko Mbagala Kuu  Mkoa wa Dar es Salaam na kusababisha maafa kwa baadhi ya wakazi.(Picha Zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO)

Mbunge wa Kigamboni,  Dk. Faustine Ndugulile (mwenye suti nyeusi) akiwasikiliza baadhi ya waathirika wa mabomu ambao  wamechukua hundi  yao ya malipo na kuwawezesha kukabati  makazi yao . Mbunge Ndugulile aliongozana na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) inayoongozwa na Mwenyekiti wake John Cheyo hayupo Pichani , Mei 22.2012.

Muathirika wa mabomu ya Mbagala yaliyotokea mwaka 2009 mkoani Dar es Salaam,  Mzee Steven  Gimongi  (kushoto) akitoa maelezo  jinsi  alivyoathirika  mbele ya Mwenyekiti wa  Kamati ya  Hesabu za Serikali (PAC), John Cheyo (mwenye koti   katikati) pamoja na ujumbe wake Mei 22,2012 walipotembelea  Mbagala Kuu na kuungalia sehemu hiyo pamoja na kuzungumza na waathirika  hao.

Baadhi ya Waathirika wa mabomu ya Mbagala wakiwa katika mkutano na  Kamati ya PAC – Mei 22.2012.

Mwenyekiti wa (PAC) John Cheyo (Mwenye koti), Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile(mwenye kaunda  suti nyeusi) pamoja na Wajumbe ya Kamati ya (PAC) na baadhi ya Uongozi wa watendaji wa serikali Mkoani DSM wakikgua baadhi ya makazi ya waathirika wa mabomu ya Mbagala Mkuu jana Mei 22.2012.

Mwenyekiti wa (PAC) John Cheyo akimwelekeza jambo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Piniel Lyimo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*