KWELI DROGBA NI KIJOGOOOO!!!!!!!!!!



HAKUNA KAMA CHELSEA ULAYA, BAYERN WALIA ALLIANZ ARENA

Allianz Arena
 Dider Drogba akishangilia.
 Didier Drogba akiwa amenyanyua juu Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kocha wa Chelsea Roberto Di Matteo akishangilia ubingwa wa Ulaya
Wachezaji wa Chelsea wakishangilia na Kombe lao.
Bastian Schweinsteiger akiwa amejifunika uso baada ya kukosa Penati ya mwisho.
Mshambuliaji Didier Drogba kushoto, akishangilia kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya sambamba na kiungo Raul Meireles na Jose Bosingwa.

LONDON, England
MSHAMBULIAJI mkongwe na nahodha wa Ivory Coats, Didier Drogba, usiku wa kuamkia leo ameipa klabu yake ya Chelsea ya England ubingwa wa Ligi ya mabingwa Ulaya 2011 - 2012 alipoifungia bao la kusawazisha na baadaye kufunga penati ya mwisho iliyosababisha wawalaze Bayern Munich ya Ujerumani kwa penati 4-3, amesema ushindi huo umeipooza machungu yao ya 2008.

Akizungumza baada ya kutua jijini London, huku wakiwa na taji la kwanza la Ligi ya mabingwa Ulaya, Drogba alisema kuwa mwaka 2008 walinyongwa sana mjini Moscow wiliposhindwa na Manchester United katika fainali kwa mikwaju ya peneti.
Alisema baada ya kucheleweshwa sana hatimaye Mwenyezi Mungu ameamua kuwapa kile alichowapangia kwa muda mrefu na ambacho walicheleweshewa kukipata na kwamba sasa roho zao zimepoa.
“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kutuwezesha kuwa mabingwa Ulaya baada ya kucheleweshewa kwa muda mrefu, kwa kweli hii ni furaha tuliyoisubiri kwa muda mrefu,” alisema Drogba aliyetokwa na machozi baada ya kufunga penalti iliyowapa ubingwa.
Katika mchezo huo wa juzi timu hizo zilimalizi dakika 90 kwa sare ya bao 1-1, Munich ndio waliokuwa wa kwanza kujipatia bao likifungwa na Thomas Müller katika dakika ya 83 lakini Didier Drogba akasawazisha katika dakika ya 88 na kusababisha timu hizo kuongezewa dakika 30 za nyongeza.
Katika dakika ya tano ya muda wa nyongeza Drogba alimkwatua Frank Ribery ndani ya eneo la hatari na mwamuzi akaizawadia penati lakini hata hivyo Arjen Robben, akashuhudia penati yake hiyo ikidakwa na kipa Petr Cech, katika dakika ya 95.
Baada ya kukosa penalti hiyo vijana wa Munich wakapoteza umakini na kujiamini na kuwapa Chelsea mwanya wa kufanya mashabulizi na kuutawala mchezo hadi dakika 15 za kwanza za muda wa nyongeza zilipomalizika na hata dakika 15 za mwisho mambo yaliendelea kuwa sare ya 1-1.
Baada ya kupigwa kura na kukukubaliana kulitumia goli la upande wa Kusini mwa uwanja, Bayern Munich ndio walioanza kupiga mikwaju ya penalti ambapo nahodha wake Philipp Lahm alifunga kabla ya Juan Mata wa Chelsea kupoteza, Mario Gomez akaifungia Munich penalti ya pili na David Luiz akaifungia Chelsea penalti ya kwanza kisha Manuel Neuer akaipa Munich penalti ya tatu na Frank Lampard akaifungia Chelsea penalti ya pili, Ivica Olic akaikosesha Munich penalti na Ashley Cole akafunga kufanya matokeo yawe penalti 3-3, Bastian Schweinsteiger akakosa penati ya tano ya Munich na Didier Drogba akafunga penati ya mwisho ya Chelsea hivyo matokeo kuwa 4-3.
Hilo limekuwa taji la kwanza Chelsea na imethibitisha kuwa ingali juu ya Bayern Munich kwani mara ya mwisho kwa timu hizi kukutana ilikuwa mwaka 2005 katika robo fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya ambapo Chelsea ilishinda kwa jumla ya mabao 6-5 ya ugenini na nyumbani.
Wachezaji wa Chelsea waliokuwa kwenye kikosi hicho wakati huo na ambao hivi karibuni waliipa taji la Kombe la FA ni pamoja na Petr Cech, John Terry, Ashley Cole, Frank Lampard na Didier Drogba ambao pia wote walishiriki katika mechi hiyo.
Kwa kipigo hicho Bayern Munich ilishindwa kuungana na Liverpool kutwaa taji hilo kwa mara ya tano ikiwa imezidiwa na Real Madrid ya Hispania na AC Milan ya Italia, Munich walishindwa kuendeleza umwamba wa klabu za Ujerumani kuzitambia zile za England zilipopambana kwenye fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya.
Aidha hilo limekuwa pigo kwa kocha wa Munich, Jupp Heynckes, ambaye alishindwa kuingia kwenye rekodi ya kuwa kocha wa 19 kushinda kombe hili mara mbili, kwani alilitwaa mwaka 1998 alipokua akiinoa Real Madrid.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI