Leticia Nyerere adaiwa kukamatwa Marekani

Kuna madai kuwa Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere (CHADEMA-Kwimba), amekamatwa nchini Marekani akikabiliwa na makosa mawili ya jinai.

Taarifa zilizosambaa sehemu mbalimbali nchini, zimedai kuwa mbunge huyo, Machi 26, mwaka huu, alitenda kosa la kupatikana na kadi ya kijani kwa njia ya udanganyifu akidaiwa kudanganya kuwa alikuwa mmoja wa waathirika wa unyanyasaji wa kifamilia.

Hata hivyo, habari hizo zinadai kuwa mbunge huyo aligundulika kusema uongo kwa vile hati yake ya kusafiria ilionyesha amefika Tanzania mara kadhaa ambapo kwa mujibu wa maelezo yake alikuwa akidai kunyanyaswa kifamilia.

Aidha mtoa taarifa huyo anadai kuwa Leticia anatuhumiwa kujipatia dola 15,000 kutoka kwa mtu aliyetajwa kwa jina la Cooper, na pia kushindwa kufika katika mahakama ya Maryland Februari 10 kusikiliza shauri hilo.
Hata hivyo, uongozi wa CHADEMA nchini Marekani umekanusha vikali tuhuma hizo na kuziita za uzushi zilizolenga kumchafua mbunge huyo machachari.

Katika taarifa yao iliyosambazwa katika vyombo kadhaa vya habari, uongozi huo umedai kuwa aliyesambaza ujumbe huo ana lengo baya na ni moja ya mbinu za wapinzani wao kutaka kukichafua chama hicho na viongozi wake.

“Tunapenda kuchukua nafasi hii kukanusha vikali taarifa iliyosambazwa kupitia mitandano ya kijamii ya kwamba Leticia Nyerere amekamatwa. Kwa kweli hizi sio taarifa za kweli, ni za uzushi na kutaka kuchafuana. Tunamlaani vikali mtu yeyote aliyehusika kusambaza taarifa hizo,” ilisema sehemu ya taarifa hizo.
Juhudi kadhaa zilizofanywa na Tanzania Daima kutaka kuwasiliana na mbunge huyo kwa njia ya simu, zilishindikana hadi tunakwenda mitamboni.


juu

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.