Lowassa awatuliza wanaCCM wasihamie Chadema

MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa, amekuwa na mikutano ya ndani katika jimbo lake katika kile kinachoonekana kuwa ni jitihada za kutuliza wimbi la wana CCM kuhamia Chadema.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wanaCCM katika mikoa mbalimbali kuhamia Chadema. Mkoa wa Arusha ndiyo unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanachama wa CCM wanaojiunga na Chadema.
Jana Lowassa ambaye aliwahi kuwa  Waziri Mkuu kabla ya kujiuzulu, alifanya mkutano wa ndani katika eneo la Mto wa Mbu na baadaye kufuatiwa na mkutano wa hadhara.

Katika mkutano huo wa hadhara, mbunge huyo aliwaambia wananachi kuwa pamoja na kuwa suala la kujiunga na chama chochote cha siasa ni haki ya mtu, lakini haoni umuhimu wa wana CCM kwa sasa kuhama chama hicho kinachotawala.

Alisema CCM  ni chama chenye kutetea maslahi ya wanyonge na kwamba kuna haja kwa wananchi kutathimini ili kuona kama kweli CCM imeshindwa kutimiza malengo yake.


Alisema CCM imekuwa ikitekeleza kwa vitendo mchango wa Baba wa Taifa Mwalimu Jiulius Nyerere ambao nni umoja na mshikamano, vinavyoifanya Tanzania kuendelea kuwa kisiwa cha amani.
Lowassa pia alisema CCM ni chama kinachotetea maslahi na rasilimali za nchi ili zisiporwe  na wageni.

Amewakumbusha kuwa CCM ni chama kinachotoa nafasi kwa wanachama wake kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa bila ya mizengwe au ubaguzi wa rangi, ukabila au dini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.