MANCHESTER CITY MABINGWA KOMBE LIGI KUU YA ENGLAND

MANCHESTER, England
MANCHESTER City wametwaa ubingwa wa kwanza wa Ligi Kuu ya England baada ya kupita miaka 44, kwa kuifunga Queens Park Rangers 3-2 katika mechi ya mwisho.

Mshambuliaji Sergio Aguero alifunga bao la tatu na ushindi katika dakika za majeruhi na kurudisha shangwe za mashabiki wa City uwanjani hapo.

Bao hilo liliingia sekunde chache baada ya Manchester United kuichapa Sunderland 1-0, hivyo ubingwa huo wa Manchester City umepatikana kwa tofauti ya mabao.

Zabaleta alifunga bao la kwanza kabla ya Edin Dzeko na Aguero waliokuwa mashujaa wa City kwenye uwanja wake wa Etihad kufunga mabao.

"Kushinda kwa aina hii ni kitu kizuri. Sijawahi kuona mechi ya mwisho ngumu kama hii. Baada ya miaka 44 tumefanikiwa kutoa zawadi kwa mashabiki wetu wote," alisema kocha wa City, Roberto Mancini.

Arsenal imemaliza nafasi ya tatu baada ya kuichapa West Bromwich Albion 3-2, wakati huo mkiani Bolton Wanderers imekuwa timu ya mwisho kushuka daraja baada ya kulazimishwa sare 2-2 na Stoke City.

Wakati huohuo;Juventus imevunja rekodi ya AC Milan ya kucheza mechi 42 bila ya kufungwa na kumaliza msimu mzima wa ligi bila ya kupoteza baada ya kushinda 3-1 dhidi ya Atalanta jana.

Pia, mechi hiyo ilikuwa ni sherehe nzuri ya kumuaga nahodha wao aliyetumiakia klabu hiyo kwa miaka19, Alessandro Del Piero, ambaye alifunga kitambaa cha unahodha kwenye mchezo huo wa mwisho wa Serie A akiwa na jezi ya Juventus pia alifunga la bao la pili kwenye mchezo huo.

Ushindi huo umeifanya Juve kucheza michezo 43 bila ya kupoteza kwenye mashindano yote msimu huu.

Hii ni mara ya kwanza katika Serie A tangu Milan ilipofanya hivyo mwaka 1992 na mara ya kwanza tangu ligi ya Italia ilipoongeza timu za kucheza ligi hiyo kutoka 18 hadi 20.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*