MAWAZIRI KUAPISHWA JUMATATU



THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


Coat of Arms
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUAPISHWA KWA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, atawaapisha Mawaziri na Naibu Mawaziri Jumatatu tarehe 7 April, 2012, saa 5 asubuhi katika viwanja vya Ikulu.

Kwa kuzingatia umuhimu wa shughuli hii, Nawaomba wahariri mtutumie majina ya waandishi waandamizi ambao watafika ikulu mapema saa 4.00 asubuhi kwa ajili ya shughuli hii.

Tunaomba majina hayo ya wawakilishi wa vyombo vyenu yawasilishwe kwetu mara baada ya kupata taarifa hii na mwisho wakupokea majina itakuwa  saa 2.00 asubuhi ya Jumatatu, kwa sababu ifikapo saa 4.00 kamili asubuhi kila mwalika anatakiwa awe tayari ameshakaa kwenye sehemu yake aliyopangiwa.

Tunapenda kusisitiza kuwa waandishi watakaoruhusiwa kuhudhuria shughuli hii ni wale tu ambao tutapokea majina yao kutoka kwa wahariri wa vyombo husika. Aidha, tunasisitiza mavazi yawe nadhifu na heshima, kwa kuwa hii ni shughuli ya Kitaifa.


Tunaomba ushirikiano wenu na karibuni.

……..Mwisho…..

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
5 Mei, 2012

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI