Moshi yapata Washindi wa Tuzo za Kili Music

Majaji wakijadiliana jambo.

Washindi wa Moshi ndio hawa Charlz Mushi, Gaspar Fadhil, a.k.a Chagga Boy na Atufigwege Mwailunga.
Baada ya mikoa ya Mwanza na Dodoma kupata wawakilishi katika shindano la kusaka vipaji vya mikoani, Kili Regional Talent Search 2012, mkoa wa kilimanjaro nao jana ulipata wawakilishi watakaoungana na washindi wa tunzo za muziki za msimu huu, katika tamasha la washindi litakalofanyika katika viwanja vya Chuo cha Ushirika tarehe 12 ya mwezi huu ambayo ni Jumamosi ya wiki hii.

Tofauti na mikoa mingine, Moshi walionekana kuwa na msukumo zaidi katika muziki wa Hip Hop pamoja na wasichana kuwa na idadi kubwa ya washiriki tofauti na mikoa mingine ambapo walikuwa hawazidi hata asilimia 5 ya washiriki wa shindano hilo.

Jumla ya watu 400 walishiriki katika mchujo wa kwanza, huku majaji wanne wakiwa katika mchakato huo uliofanyika katika ukumbi wa sinema wa Mr Price, na hatimaye mpaka kufika mchujo wa pili, ni watu 47 tu walikuwa wamepatikana kuingia nusu fainali.

Wakiongelea mchakato huo, kila mtu kwa wakati wake, majaji wa shindano hilo waliutaja mkoa wa KIlimanjaro, na hasa wilaya ya Moshi kwamba ni sehemu ambayo walifanya kazi kwa urahisi ukilinganisha na mikoa mingine.

Ila kama ilivyotegemewa Moshi umekuwa mkoa wa kwanza kutoa mwanamuziki mwenye kipaji cha Hip Hop jambo ambalo limekuwa faraja sana kwa mwanamuziki wa kizazi kipya anayeongoza jopo hilo la Majaji, Joseph Haule a.k.a Professor Jay.

Tofauti na mikoa mingine, Moshi pia ndio kituo pekee ambacho, licha ya wasichana wengi kujitokeza kushiriki, hakuna hata msichana mmoja aliyefanikiwa kufikia hatua ya ushindi, na kupata nafasi ya kushiriki tamasha la washindi litakalofanyika Jumamosi hii.

Mchakato wa majaji umewataja Gasper Fadhil a.k.a Chagga Boy, Charl Mushi, na Atufigwege Mwailunga kuwa wawakilishi wa mkoa wa Moshi.

Washiriki hawa watapata nafasi ya kila mmoja wao kurekodi wimbo mmoja na kisha wote kurekodi wimbo wa pamoja, ambazo wataziimba mbele ya mashabiki wa mkoa wao siku ya Tamasha la washindi.

 
Mmoja kati yao atakayefanya vizuri zaidi, atashiriki katika tamasha kubwa la washindi litakalofanyika mkoani Dar, mapema mwezi ujao.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU