Msondo Ngoma 'kuwasha moto' Masasi mkoani Mtwara Juni 2.

Na Mwandishi Wetu

BENDI Kongwe ya Msondo Ngoma ya jijini Dar es salaam inatalajia kufanya uzinduzi wa ukumbi mpya kabisa wa kisasa wa burudani  wa Emirate Hall uliopo Masasi June 2 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila 'Super D' Alisema wamealikwa kwa ajili ya kutoa burudani siku ya ufunguzi wa ukumbi huo ambapo watatoa burudani isiyo na kifani

"Unajua sisi ni baba ya muziki nchini ndio maana wapenzi wengi wanahitaji burudani kutoka kwetu ndio mana tunapopata nafasi ya kwenda mikoani tunakwenda kama hivi tumealikwa kutoa burudani siku hiyo tutatoa burudani ya uwakika" Mhamila.

Siku hiyo tutapiga vibao vetu vya zamani na vipya kwa sasa alivitaja baadhi ya vibao vitakavyonogesha uzinduzi huo kuwa ni Suluhu wa Shabani Dede, Nadhiri ya Mapenzi wa Juma Katundu na Baba Kibene wa Eddo Sanga hizo ni baadhi ya nyimbo mpya zitakazonogesha siku hiyo vile vile watapiga nyimbo zao za zamani zilizotamba wakati huo.

Kundi hilo litaambatana na wanamuziki wake wote wakiwemo wakongwe katika muziki wa Dansi nchini Maalimu Gulumo ' Kamana', Saidi Mabela ' DKT Mabela' na wengine wote watafanya vitu vyao siku hiyo kwa ajili ya kukonga nyoyo za mashabiki wao wa Masasi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.