NGORONGORO YAING'OA SUDAN, ULIMWENGU SHUJAA

Ulimwengu, mfungaji wa bao la Ngorongoro
TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes imefanikiwa kusonga mbele katika kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika usiku huu, baada ya kutioa Sudan kwa jumla ya mabao 4-3.

Ngorongoro leo imekubali kichapo chepesi cha mabao 2-1 ugenini, kwenye Uwanja wa Khartoum, baada ya awali kushinda 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wiki mbili zilizopita na sasa itachuana na Nigeria Raundi ya Pili, mechi ya kwanza ikicheza Julai 28, mwaka huu Dar es Salaam.
Sudan walipata mabao yao kupitia kwa Mohammed Abdelrahman dakika ya 10 na Ahmad Nasr kwa penalti dakika ya 65, wakati bao la Ngorongoro lilifungwa na mshambuliaji wa Tout Puissant Mazembe ya DRC, Thomas Emmanuel Ulimwengu kabla ya mapumziko.
Ngorongoro Heroesinatarajiwa kurejea nchini Jumapili (leo) majira ya Saa 3 asubuhi.
Mshindi kati ya Ngorongoro na Nigeria atamenyana na mshindi kati ya Afrika Kusini na Kongo Brazzaville, mechi ya kwanza ikichezwa kati ya Septemba 21 na 23 mwaka huu ugenini na marudiano Oktoba 6.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*