NHIF anzisheni TIKA haraka-Madiwani

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Kheri Kessy akifungua mafunzo ya uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii (TIKA) yaliyohusisha Kamati ya Mipango na Fedha na Kamati ya Huduma za Jamii.

Na Mwandishi Wetu
MADIWANI wa Manispaa ya Ilala wameutaka Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya (NHIF) na Uongozi wa Manispaa hiyo kuharakisha
taratibu za uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii (TIKA) ili
wananchi wawe na uhakika wa matibabu.

Agizo hilo lilitolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa
Kamati ya Huduma za Jamii Bi. Angelina Malembeka baada ya
kumalizika kwa mafunzo ya uanzishaji wa Mfuko huo.

Alisema kuwa mpango huo ni mzuri na unalenga moja moja kwa
moja kumsaidia mwananchi hivyo wakiwa kama wawakilishi wa
wananchi watalipa kipaumbele jambo hilo hasa baada ya kufika
katika ngazi ya kutoa maamuzi.

"Jambo la afya ni suala nyeti sana ambalo tunapaswa kulipa
msukumo mkubwa, hivyo NHIF na Watendaji katika Manispaa
yetu harakisheni mchakato huu na litakapofika kwetu tutalipa
msukumo kwa manufaa ya wananchi wetu," alisema
Malembeka.

Awali baadhi ya madiwani walihoji ni kwa namna gani Mfuko
huo umejipanga kutoa huduma kwa wanachama watakaojiunga
au kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa dawa katika
vituo vya kutolea huduma.

Akijibu maswali yaliyohojiwa, Mkurugenzi wa Uhai wa Mfuko,
Bw. Michael Mhando alisema kuwa usimamizi mkubwa wa
huduma zitolewazo na mfuko huo ziko kwenye Manispaa husika
chini ya Bodi za Huduma za Afya za Manispaa utaratibu
utakaowezesha kujipanga na kusimamia vyema ubora wa
huduma kwa wanachama.

Suala jingine ambalo lilihojiwa ni wigo wa huduma hiyo kwa
wanachama ambapo walitaka kujua kama utaweza kumhudumia
mwanachama nje ya nchi, Katika hilo, Bw. Mhando alisema
kuwa utaratibu wa kutibu wanachama nje ya nchi haupo kwa
sasa na kinachofanywa na NHIF ni kuboresha na kujenga uwezo
wa vituo vya kutolea afya vya ndani ili viweze kutoa huduma
bora.

Akielezea umuhimu wa Tiba kwa Kadi, Bw. Mhando alisema
kuwa utasaidia kutatua changamoto ya upandaji wa gharama za
matibabu na kupunguza mzigo wa Manispaa wa kutoa huduma
za matibabu kwa makundi maalum.

"Mbali na umuhimu huo, TIKA itasaidia kuongezeka kwa
rasilimali fedha katika utoaji wa huduma za Afya ili kukabiliana
na changamoto za upatikaji wa dawa na vifaa tiba lakini pia
ushirikishaji wa wananchi katika kuchangia huduma za afya na
kujiletea maendeleo," alisema.
 



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*