NHIF yaendesha mafunzo ya mtindo bora wa maisha

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF akimjulia hali mwanachana wa Mfuko huo alipotembelea Hospitali ya Mkoa wa Kigoma kwa lengo la kuona wanachama hivi karibuni.
 Na Mwandishi Wetu
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Ujerumani (GIZ ) na Counsenuth unaendesha mafunzo ya siku nane kuhusu mtindo bora wa maisha na lishe bora kwa Wizara na Taasisi mbalimbali nchini ili kusaidia kuepukana na maradhi yasiyo ya kuambukiza kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo kwa Watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Meneja wa Kanda ya Ilala wa NHIF, Raphael Mwamoto alisema mafunzo hayo yanalenga kuwaelimisha wananchi kuhusu namna ya kutambua viashiria vya maradhi yanayotokana na mtindo wa maisha ambayo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi katika siku za hivi karibuni.
“ NHIF haishughulikii tu matibabu ya wanachama wake, inapenda pia kuona wanachama wake wanakuwa na elimu juu ya kujikinga na maradhi yasiyo ya kuambukiza au yanayosababishwa na mtindo wa maisha kama kula na mambo mengine”. Alisema Mwamoto.
Aliongeza kuwa matibabu ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza yamekuwa yakigharimu fedha nyingi hivyo NHIF imeona ni vema kukabiliana nayo kwa kutoa elimu ya mtindo bora wa maisha badala ya kusubiri wanachama wake waugue na kutumia fedha nyingi kuwatibu.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo Selestine Kisimba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo amewahimiza watumishi wa Wizara hiyo kujenga tabia ya kufanya mazoezi na kupima afya zao mara kwa mara ili kujiepusha na maradhi yasiyo ya lazima.
Amesema maradhi kama shinikizo la damu, kisukari na kiharusi yanaweza kuepukika kama kila mmoja atatenga muda wa kufanya mazoezi angalau mara moja kwa wiki.
Kisimba aliongeza kuwa mtindo wa maisha na kazi za kila siku hautoi nafasi kwa watumishi wa umma kufanya mazoezi ya viungo hivyo ni vema kila idara ikatenga siku maalumu kwa ajili ya mazoezi kwa watumishi wake.
Pamoja na mafunzo hayo huduma za upimaji wa kisukari, hali lishe, shinikizo la damu na Virusi vya Ukimwi (VVU) pia zinatolewa kwa watumishi wanaoshiriki mafunzo hayo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.