PONGEZI DK. REGINALD ABRAHAM MENGI- TOKA ACCRA, GHANA.


Kwa niaba ya Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF), Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC) pamoja na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) na kwa niaba yangu binafsi ninapenda kuchukua fursa hii adimu kumpongeza Dk. Reginald Abraham Mengi kwa kutunukiwa tuzo ya Biashara na Amani  kati ya watu mashuhuri duniani!
Dk. Reginald Abraham Mengi amekuwa chachu ya maendeleo na mafanikio ya biashara kwa watanzania na waafrika wote katika kipindi cha miaka zaidi ya ishirini iliyopita. Juhudi zake za kujenga amani kupitia uchangiaji wa uchumi katika nchi za Afrika pamoja na moyo wake wa kupenda sana watu ni nadra sana kuziona kwa watu wengi.
Tuzo aliyopata Dk. Reginald Abraham Mengi imeifanya Tanzania na bara zima la Afrika lionekane kuwa moja ya familia imara za kimataifa. Tuzo hii imeifanya Afrika ionekane kuwa inayoweza kutoa watu wenye akili pamoja na mioyo ya kupenda na kutengeneza mazingira ya kufanikiwa kwenye biashara. Ni tuzo iliyoliinua bara la zima la Afrika juu zaidi na kulifanya lione fahari ya kuheshimika.
Sisi sote tumezoea kuwaona wazungu na watu kutoka Asia wakitunukiwa tuzo mbalimbali za kimataifa zenye hadhi kama aliyopewa Dk. Reginald Abraham Mengi lakini ni nadra sana kuona tuzo kama hizi zikitolewa kwa Waafrika.
Watu wa aina ya Dk. Reginald Abraham Mengi wapo wachache sana na natamani tungekuwa nao kwenye serikali za kiafrika ili waweze kufanya kazi kwa manufaa na maendeleo ya bara la Afrika.
Nimekuwa katika jiji hili la Accra, Ghana kusimamia mpambano wa ngumi la IBF la mabara na nimefarijika sana kuona watu wa rika zote pamoja na jinsia zote wakiifurahia tuzo hii kama vile amepewa Mghana mwenzao. Kila mtu hapa Accra anamtaja Dk. Reginald Abraham Mengi kama mwenzao (Mwaafrika) bila kutaja utaifa wake!
Hongera sana Dk. Reginald Abraham Mengi kwa kuifanya Afrika ing’are kwenye uso wa dunia.
Hongera sana Dk. Reginald Abraham Mengi kwa kugusa USO wa DUNIA kwa jina lako TUKUFU!
Sote tunakupenda na tunakuombea mungu azidi kukulinda na kukupa kheri na fanaka uzidi kuing'arisha Afrika na dunia yote!

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA