Rais Kikwete amlilia Patrick Mafisango

Rais Jakaya Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Mwenyekiti wa Klabu ya Soka ya Simba ya Dar es Salaam, Mheshimiwa Ismail Aden Rage, kuomboleza kifo cha mchezaji wa klabu hiyo Marehemu Patrick Mafisango.
 
Mchezaji Mafisango alipoteza maisha wakati gari alilokuwa anaendesha lilipopata ajali katika eneo la Chang’ombe, Dar es Salaam, usiku wa kuamkia jana, Alhamisi, Mei 17, 2012.
 
Katika salamu zake za rambirambi, Rais Kikwete amesema kuwa ameshtushwa na kuhuzunishwa na upotevu wa maisha ya mchezaji huyo ambaye katika miaka yake michache ya uchezaji katika Tanzania amechangia maendeleo ya soka nchini kupitia klabu yake ya Simba.

“Nimepokea kwa mshtuko na huzuni habari za upotevu wa maisha ya Patrick Mafisango katika ajali ya gari ambayo nimejulishwa ilitokea asubuhi ya kuamkia jana katika eneo la Chang’ombe mjini Dar Es Salaam,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

“Nakutumia wewe Mheshimiwa Mwenyekiti salamu zangu za rambirambi kufuatia msiba huu mkubwa kwa Klabu ya Simba na wanamichezo wote nchini. Nakuomba kupitia kwako uwafikishie salamu zangu za rambirambi za dhati kabisa wana-familia wote wa Marehemu Mafisango, Wana-Simba wote popote walipo na wanamichezo wa Tanzania kwa jumla.”

Ameongeza Mheshimiwa Rais Kikwete: “Wajulishe wote kuwa niko nao katika msiba huu mkubwa. Aidha, wajulishe kuwa naungana nao katika kumwomba Mweyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aiweke mahali pema peponi roho ya Marehemu Patrick Mafisango . Amen.”
 ……..Mwisho….
 
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
18 Mei, 2012

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI