Rais Kikwete ateua Wakurugenzi Wapya Tisa wa Wizara ya Mambo ya Nje

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameteua Wakurugenzi wapya tisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambao pia watakuwa na hadhi ya Balozi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mjini Dar es Salaam leo, Jumatano, Mei 30, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi huo umeanza Mei 2, mwaka huu, 2012.

Walioteuliwa ni Ndugu Vincent Kibwana ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Afrika; Ndugu Naimi Aziz ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda; Ndugu Celestine Mushy ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa; Ndugu Yahya Simba ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Mashariki ya Kati, na Ndugu Bertha Somi ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Diaspora.
 
Wengine ni Ndugu Irene Kasyanju aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi, Kitengo cha Sheria; Ndugu Dorah Msechu ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Ulaya na Amerika, Ndugu Mbelwa Kairuki ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Asia na Australia, na Ndugu Silima Haji ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Mambo ya Nje, Zanzibar.

Kabla ya uteuzi wake,  Ndugu Kibwana  alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu, Ndugu Naimi Aziz alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ndugu Mushy alikuwa Kaimu Katibu wa Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ndugu Simba alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu, na Ndugu Somi alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu.

Naye Ndugu Kasyanju alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ndugu Msechu alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ndugu Kairuki alikuwa Msaidizi wa Rais (Hotuba), Ofisi ya Rais, Ikulu na Ndugu Haji alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu.    
                                ..……..Mwisho……….

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA