Rukwa Waadhimisha Miaka 10 Ya NHIF

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akihutubia wadau wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoani Rukwa katika ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga jana. Katika hotuba yake hiyo aliutaka mfuko kuboresha huduma zake mara kwa mara na kuhakikisha wanawafikia wananchi wengi zaidi kujenga uelewa wa mfuko na faida zake ili waweze kujiunga. Aidha aliutaka mfuko kushughulikia malalamiko yote yanayotolea na wadau juu ya huduma zinazotokana na mfuko kwa ustawi wa mfuko na jamii kwa ujumla. Mfuko wa Bima ya Afya nchini unaadhimisha miaka 10 ya kujituma na kuaminiwa ambapo kaulimbiu yake ni "Huduma za matibabu vijijini na huduma bora za afya kwa wote
Wadau wa Mfuko wakifuatilia mada mbalimbali katika kikao hicho.
Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na wadau wa mfuko wa NHIF jana katika ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga. Kulia ni Mganga Mkuu Hospitali ya Mkoa wa Rukwa Dkt. Gurisha John William, Afisa Tawala Mkoa wa Rukwa Festo Chonya, Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Mkoa wa Katavi Lauteny Kanoni, Mjumbe wa Bodi ya NHIF, Naibu Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa Bima ya Afya Nchini Hamis Mdee na Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa.
Wataalamu wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini ambao walikuwa Sekretarieti ya kikao hicho wakiwa kazini.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini Ndugu Hamis Mdee akizungumza kwenye mkutano huo. Alisema lengo kubwa la kufanya ziara Mkoani Rukwa ni kutoa taarifa za mfuko wa bima ya afya na mfuko wa afya ya jamii pamoja na kuelezea umuhimu wa mifuko hiyo kuhamasisha jamii kujiunga ili kuongeza ushiriki katika mifuko hiyo.
Na Ndg,Temba.Sumbawanga

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI