Sabodo atoa bilioni 5/- kujenga jengo la kuegesha magari


Na Dotto Mwaibale
 
MFANYABIASHARA maarufu nchini, Mustafa Sabodo ametoa zaidi ya sh.bilioni 5 kwa madhehebu ya Khoja Shia Ithnaashri Jamat kwa ajili ya kujenga jengo la maegesho ya magari.
Akizungumza katika hafla ya kupokea vibali vya ujenzi wa jengo hilo Dar es Salaam leo kutoka kwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa alisema jengo hilo litasimamiwa na madhehebu hayo.
Alisema jengo hilo lililopo katika mitaa ya India na Morogoro la ghorofa 14 litakuwa na uwezo wa kuhifadhi magari 180 kwa wakati mmoja.
Silaa alisema fedha zitakazopatikana kwa malipo ya maegesho ya magari katika kipindi cha miaka 10 zitafanya kazi ya kuchimba visima katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.
Meya alisema kwa muda mrefu Jiji la Dar es Salaam limekuwa likikabiliwa na maeneo ya kuegesha magari na kuwa jengo hilo la kwanza kubwa litakuwa ni mkombozi mkubwa.
"Kwa muda mrefu tumekuwa na matatizo ya kuegesha magari katika jiji letu hivyo msaada aliotoa ndugu yetu Sabodo kwa madhehebu hayo ya ujenzi wa maegesho hayo itasaidia sana kupunguza tatizo hilo," alisema Silaa.
Alisema Manispaa imepokea jambo hilo kwa mikono miwili na ndio maana imekamilisha vibali ili ujenzi huo uende pasipo kikwazo chochote.
Alisema jengo hilo litaitwa Sabodo Car Park jambo litakalo weka kumbukumbu ya mchango wake katika kufanikisha shughuliza za maendeleo.
Mwenyekiti wa Madhehebu hayo Shiraz Walji, alimshukuru Sabodo kwa msaada wake huo na kuahidi kusimamia vizuri mradi huo ambao utakuwa wa manufaa kwa Watanzania wote.
 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI