SAMATTA, ULIMWENGU WAJIUNGA KAMBI YA TAIFA STARS

MBWANA SAMATA, ULIMWENGU
Washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaocheza mpira wa kulipwa katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wamejiunga na kambi ya timu ya Taifa (Taifa Stars) jana (Mei 21 mwaka huu).
Wachezaji hao ambao ndiyo pekee kutoka nje walioitwa na Kocha Kim Poulsen kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast itakayochezwa Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan waliwasili jana saa 1.30 usiku kwa ndege ya Kenya Airways.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inaendelea na mazoezi jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Karume na Taifa itacheza mechi ya kirafiki Mei 26 mwaka huu dhidi ya Malawi. Mechi hiyo itafanyika Uwanja wa Taifa, na Malawi itawasili nchini Mei 24 mwaka huu.
Baadaye Malawi itakwenda Zanzibar kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Zanzibar Heroes itakayofanyika Mei 28 mwaka huu kabla ya kuondoka Mei 30 mwaka huu kwenda Uganda ambapo Juni 2 mwaka huu itcheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika.
TWIGA STARS KWENDA ETHIOPIA MEI 24
Timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) inatarajia kuondoka nchini Mei 24 mwaka huu kwa ndege ya Ethiopian Airlines kwenda Addis Ababa kwa ajili ya
mechi ya mchujo ya Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Ethiopia. Mechi hiyo itachezwa Mei 27 mwaka huu.
Msafara wa Twiga Stars utakuwa na watu 25 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi. Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Lina Kessy ndiye atakayeongoza msafara huo.
Twiga Stars itarejea nyumbani Mei 28 mwaka huu kusubiri mechi ya marudiano itakayochezwa Juni 16 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mshindi ndiye atakayepata tiketi ya kucheza Fainali za Nane za AWC zitakazochezwa Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.
TWIGA STARS, BANYANA ZAINGIZA MIL 8/-
Mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Twiga Stars na Afrika Kusini (Banyana Banyana) iliyofanyika Mei 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 8,012,000.
Mapato hayo yametokana na washabiki 6,418 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 1,000, sh. 5,000 na sh. 1,000. Washabiki 6,057 walikata tiketi z ash. 1,000.
Asilimia 18 ya mapato ambayo ni sh. 1,222,169 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh. 1,560,000), waamuzi (sh. 650,000), usafi na ulinzi (sh. 1,000,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing Construction (sh. 500,000) na umeme (sh. 300,000).
Kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 475,966, asilimia 10 ya uwanja sh. 237,983, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 118,992 na asilimia 65 ya TFF (sh. 1,546,890).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Powered by Sorecson : Creation de site internet

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.