SBL,NMB ZAIPIGA JEKI TWIGA STARS

BENKI ya NMB na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) jana zimetoa sh.milioni 30 kwa timu ya timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) inatarajia kuondoka nchini kesho jioni Ethiopia kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya timu ya Taifa ya nchi hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam leo wakati wa kukabidhi Menka huu kwa ndege ya Ethiopian Airlines kwenda Addis Ababa kwa ajili ya  mechi ya mchujo ya Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Ethiopia. Mechi hiyo itachezwa Mei 27 mwaka huu.

Msafara wa Twiga Stars utakuwa na watu 25 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi. Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Lina Kessy ndiye atakayeongoza msafara huo.

Twiga Stars itarejea nyumbani Mei 28 mwaka huu kusubiri mechi ya marudiano itakayochezwa Juni 16 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mshindi ndiye atakayepata tiketi ya kucheza Fainali za Nane za AWC zitakazochezwa Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI