SEMINA YA WAPIGA PICHA ZA HABARI YAFANYIKA DAR

 Mwandaaji wa semina ya siku mbili ya upigaji picha za habari wa wapiga picha za habari waandamizi, Selemani Mpochi (kushoto) akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo iliyodhaminiwa na Airtel Tanzania pamoja na Benki ya CRDB, Dar es Salaam leo. Katikati ni mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tganzania (TMF), Ernest Sungura na ofisa wa Airtel.
 Wapiga picha waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wakisikiliza kwa makini wakati Ernest Sungura wa TMF.
Mkufunzi kutoka Taasisi ya  Frame Tree Media Trust, Mwanzo Millinga (kulia) akitoa mafunzo kuhusu upigaji picha za habari, wakati wa semina ya siku mbili ya wapiga picha za habari waandamizi, iliyoandaliwa na MPS2011 Entertainment, Dar es Salaam leo. Semina hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya simu ya Airtel pamoja na Benki ya CRDB.  (NA MPIGAPICHA WETU)
 Mgeni rasmi katika semina hiyo, Ernest Sungura wa TMF (wa pili kulia mbele), akiwa katika picha ya pamoja na wanasemina baada ya kufungua semina hiyo leo katika moja ya kumbi za Msimbazi Centre, Dar es Salaam.
 Mpiga picha mwandamizi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Bashir Nkoromo (kulia) ambaye pia ni Mtayarishaji Mkuu wa Blogu za Nkoromo Daily na CCM,  akijadiliana jambo na Mpiga picha Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda (kushoto) pamoja na Mgeni rasmi Ernest Sungura kutoka TMF. Mwaikenda pia ndiye Mtayarishaji Mkuu wa Blogu hii ya Kamanda wa Matukio
Mgeni rasmi katika semina hiyo, Ernest Sungura wa TMF (wa pili kulia mbele), akiwa katika picha ya pamoja na wanasemina baada ya kufungua semina hiyo leo katika moja ya kumbi za Msimbazi Centre, Dar es Salaam.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA