Serikali Yapiga Marufuku Mikusanyiko Yote isiyokuwa na Kibali
Na Juma Mohammed,MAELEZO
Zanzibar Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepiga marufuku mikusanyiko ya aina yoyote ikiwemo mihadhara ya aina mbalimbali ambayo hajapata kibali cha Serikali.
Akitoa taarifa ya Serikali,Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ,Mohammed Aboud Mohammed amesema mbali na suala hilo,pia imewataka wananchi kuheshimu sheria.
Waziri Aboud amesema pia Serikali imeliagiza Jeshi la Polisi kuwatafuta na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote waliohusika na fujo zilizotokea jana na leo katika mji wa Zanzibar. “Serikali inakemea vikali vitendo vyote vya hujuma na uharibifu wa mali zilizofanywa katika taasisi za umma,Dini na watu binafsi” Alisisitiza Waziri huyo.
Comments