SIMBA ITAKAVYOSHEREHEKEA USHINDI DAR LIVE JUMAPILI

Makamu Mwenyekiti wa Simba SC Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, akizungumzia maandalizi ya sherehe hiyo.
 
KLABU ya mpira wa miguu ya Simba leo imezungumzia juu ya sherehe ya ubingwa wa kombe la Tanzania bara 2012 walilolitwaa hivikaribuni.
Akizungumza na waandishi wa habari, Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, alisema maandalizi ya sherehe hiyo tayari yameshakamilika na kinachosubiriwa hadi sasa ni siku husika ambayo ni Jumapili ya wiki hii, tarehe 27.
Alisema wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo watatakiwa siku ya Jumapili hii kukusanyika makao makuu ya klabu hiyo, Mtaa wa Msimbazi, asubuhi tayari kwa safari ya kuelekea katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam, ambapo sherehe hizo zitafanyika.
Mmoja wa waratibu wa sherehe hiyo wa Dar Live, Luqman Maloto (kulia), akielezea jinsi walivyojiandaa kufanikisha sherehe hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini maelezo ya Nyange katika ukumbi wa klabu hiyo uliopo Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo, jijini Dar. Kwa hisani yaFull Shagwe Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI