Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda apokea mitambo ya kisasa ya kutengenezea barabara na miundombinu mingine kwa ajili ya Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimsikiliza kwa makini Afisa Mauzo Mwandamizi wa kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd Mhandisi Juma Hamsini alipokuwa akielezea ubora wa mitambo ya kampuni hiyo kabla ya kumkabidhi rasmi Mhe. Spika kwa ajili ya Halmashauri ya Mji wa Njombe. Mitambo hiyo imenunuliwa kwa gharama ya zaidi ya Milion 700 za Kitanzania  kwa makubaliano ya mkopo usiokuwa na riba kutoka Mfuko wa Halmashauri ya Mji wa Njombe.  Kulia kwa Mhe. Spika ni Mwenyekiti wa Kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd Mehboob Karmali na walioko kushoto ni watendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo wakiongozwa na George Mkindo (mwenye koti)Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Njombe George Mkindo akitoa pongezi zake kwa kampuni ya uuzaji wa mitambo ya ujenzi ya GF Trucks & Equipment Ltd baada ya kukubali kuizia Halmashauri yake Mitambo ya kutengenezea barabara na miundombinu mingine katika Halmashauri ya Mji wa Njombe kwa Mkopo usio kuwa na Riba wa kiasi cha Million 700 za Kitanzania

Spika wa Bunge akitoa shukrani zake kwa uongozi wa Kampuni ya  GF Trucks & Equipment Ltd kwa kuiwezesha Halmashauri ya Mji wa Njombe kupata Mitambo hiyo.
 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akijaribu mojawapo ya mitambo hiyo mara baada ya kukabidhiwa rasmi kwa ajili ya Halmashauri ya Mji wa Njombe.  Pembeni yake ni Mkurugenzi wa kamapuni ya uuzaji mitambo hiyo ya Jijini Dar es Salaam ya GF Trucks & Equipment Ltd Bw. Imran Karmali
 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifurahia mojawapo ya mitambo ya kisasa ya kutengenezea barabara na miundombinu mingine iliyonunuliwa na Halmashauri ya Mji wa Njombe kutoka Kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa kamapuni hiyo Imran Karmali, Mwenyekiti wa Kampuni  hiyo Bw. Mehboob Karmali na  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Njombe George Mkindo
  Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkabidhi mfano wa Ufunguo wa Mitambo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Njombe George Mkindo mara baada ya kuipokea kutoka kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd ambayo ndio walioiuzia Halmashauri hiyo mitambo hiyo.
Makinda akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kupokea mitambo hiyo
Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA