TAARIFA KWA UMMA – TAMKO LA J. NASSARI KUHUSU HOTUBA YAKE NMC

*TAARIFA KWA UMMA* Ninalazimika kutoa tarifa hii ili kutolea ufafanuzi mambo kadhaa hususani… hotuba yangu niliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya NMC Arusha siku ya jumamosi Tarehe 5, Mei 2012 ambapo tuliwapokea na kuwakabidhi kadi maelfu ya wanachama wapya waliojiunga CHADEMA kutokea vyama mbalimbali vya siasa hususani chama tawala CCM.
Kumetokea sintofahamu kubwa kuhusu sehemu ya hotuba yangu niliyoitoa. Ningependa ifahamike kwamba kama mwanasiasa kijana na kama mwanchama wa CHADEMA, Chama ambacho siku zote kimekuwa mstari wa mbele kuunganisha umma wa Watanzania wote katika kudai haki, umoja, amani na maendeleo ya kweli bila kujali ukanda, udini, wala historia. Ninapenda ifahamike kwamba sina nia malengo wala dhamira ya kuwagawa Watanzania kwa namna yoyote ile, kama ambavyo imekuwa ikitafsiriwa.
Hata hivyo, Mwenyekiti wangu wa Taifa alitoa ufafanuzi siku ileile kuhusu badhi ya mambo ambayo yangeweza kulete utata, napenda ifahamike kwamba alichokisema Mwenyekiti ndio msimamo wangu japokuwa baadhi ya watu wenye nia mbaya wamekuwa wakijaribu kupotosha kwa kutoa tafsiri ambayo si sahihi ili kunichafua mimi na chama changu. Ili kuweka kumbukumbu sawasawa nililieleza jeshi la polisi tafsiri ya hotuba yangu nilipofanyiwa mahojiano. Lengo la hotuba yangu lilikuwa kuweka msisitizo ili serikali na jeshi la polisi lishughulikie matatizo makubwa ya muda mrefu mbayo hayajatafutiwa ufumbuzi mpaka kupelekea baadhi ya watu kupoteza maisha, na sio kuchochea vurugu au kumzuia Rais kutekeleza wajibu wake
Joshua Nassari (MB)
Mei 09, 2012.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.