TAIFA QUEEN YACHUKUA USHINDI WA PILI MICHUANO YA AFRIKA NETIBOLI

Mke wa Makamu wa Rais  Mama Asha Bilal wa nne kutoka kushoto na mama Tunu Pinda wanne kutoka kulia pamoja na wake wa viongozi mbalimbali  wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya taifa ya Netiboli Taifa Queen mara baada ya kukabidhiwa kombe lao la ushindi wa pili katika michuano ya Afrika ya Netiboli,  baada ya Malawi kuchukua ubingwa huo, fainali hizo zilifanyika jana kwenye uwanja wa Taifa wa ndani na kufuatiwa na hafla fupi nyumbani kwa Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.
Hata hivyo fainali hizo zilichelewa kuanza kutokana na hali ya hewa ambapo muda mwingi mvua ilikuwa ikinyesha na kufanya waandaaji kuhamisha uwanja wa kuchezea mara kwa mara kutoka uwanja mkubwa  wa Taifa na uwanja wa ndani
Crew ya Fullshangwe  inamushukuru sana mama Tunu Pinda kwani juhudi zake zimeonyesha matunda na ni wazi kwamba hata wachezaji wa timu hiyo ya Taifa Queen wamefurahia sana michuano hii na wanajiona kwamba kweli walikuwa wakiwakilisha taifa, lakini pia watanzania wakiongozwa na mama Tunu Pinda pamoja na kamati yake walikuwa nyuma yao, Hongera sana mama kwa kutoa zawadi nono kwa wachezaji
 Mashabiki na wanafunzi mbalimbali wa shule ya Filbert Bayi wakishuhudia mchezo huo.
 Kutoka kulia ni Patrick Nyembea wa EATV, Nandi Mwiyombela Meneja Miradi Endelevu na Uwajibikaji kampuni ya bia ya Serengeti SBL na Jamal Bayser wa Superdoll pamojana nwadau wengine wakishuhudia mchezo huo..
 Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya bia ya Serengeti SBL Teddy Mapunda akipozi kwa picha na baadhi ya wake wa viongozi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI