TASWA YAOMBOLEZA KIFO CHA MAFISANGO NA MZEE LIMONGA

TASWA imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha kiungo wa timu ya Simba ya Dar es Salaam na mchezaji wa timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi), Patrick Mutesa Mafisango (pichani), kilichotokea  alfajiri ya Alhamisi kwa ajali ya gari jijini Dar es Salaam.
 TASWA inatoa pole kwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage, wachezaji wa timu hiyo, mashabiki na Watanzania kwa ujumla kutokana na msiba huo mkubwa kwa familia ya mpira wa miguu.
 Tunaamini waandishi wa habari za michezo wameguswa kwa kiasi kikubwa na msiba huo, kwani wakati wa uhai wake marehemu alikuwa na ushirikiano mkubwa na wanahabari na hakuwa mtu mwenye maringo, kiasi cha kushindwa kutoa ushirikiano kwa wenzake.
 Tunasema kifo chake ni pigo si kwa  Simba na familia yake tu, bali hata kwa timu ya Taifa ya Rwanda na Wanyarwanda wote, ambao pia tunawapa pole kwa msiba huo.
 Tunawapa pole wanamichezo wote na kuwaomba wawe na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu, huku wakiamini waandishi wa habari za michezo tupo nao pamoja katika majonzi hayo na kumuomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peoni. Amina.
 Kifo cha Mzee Limonga
Tunapenda kuwajulisha waandishi wa habari za michezo wote pamoja na wadau wengine kuwa mtangazaji wa habari za michezo wa Redio Uhuru, Limonga Justine, amefiwa na baba yake mzazi jana Alhamisi asubuhi kwenye hospitali ya Temeke, Dar es Salaam.
Msiba upo Mbagala kwa Mangaya, Dar es Salaam na maziko yanatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi. Naomba tuungane naye mwenzetu katika kipindi hiki kigumu kwake na tumfariji kwa kadri tuwezavyo kwa kuondokewa na mzazi wake. Nambari yake ya simu ni 0713-604578.
 Imetolewa na:
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
18/05/2012.
0713-415346

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI