TIGO YAZINDUA HUDUMA MPYA YA XTREME PACK

 Meneja Huduma wa Malipo ya kabla wa Tigo, Suleimani Bushagama (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu uzinduzi wa huduma mpya ya 'XTREME PACK' ambapo mteja  ataandika maneno hayo na kutuma kwenye namba 15509 ambapo atakatwa sh. 450 na kupata dakika 15 za bure na kutuma meseji 100 na 50MB zitakazomwezesha kuperuzi inteneti kwa saa 24. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa Tigo, Alice Maro. Picha na Kamanda Mwaikenda
Meneja Uhusiano wa Tigo, Alice Maro (kushoto), akifafanua jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika leo asubuhi Makao Makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Kijitonyama Dar es Salaam.

23 Mei, 2012, Dar es Salaam. Tigo imetangaza uzinduzi wa promosheni inayoipa pesa yako thamani, ijulikanao kama ‘Xtreme Pack’, kwa ajili ya mawasiliano ya jumla, yanayopatikana muda wowote na wakati wowote.

Kwa kupiga *148*01# au kutuma neno XTREME kwenda namba 15509, wateja wa huduma ya kulipia kabla watafurahia huduma za thamani ambazo ni pamoja na dakika 15 za muda wa maongezi zitakazowawezesha kupiga simu Tigo kwa Tigo, sms 100, 50 MB kwa ajili ya kuperuzi facebook, kutumia mtandao, E-mail pamoja na Twitter, vyote hivyo kwa gharama ya Tsh 450 na kuokoa Tsh 4,600! Pia tigo itatuma ujumbe mfupi wa maneno bure kwa wateja wao, kuwataarifu juu ya ukomo wa matumizi ya vifurushi vyao na kuwaruhusu kujiunga tena kama watahitaji .

“Tunatafuta njia thabiti ya kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma zinazoendana na thamani ya pesa zao” alisema Alice Maro ambaye ni afisa uhusiano wa Tigo. “Kwa kupitia promosheni hii mpya wateja wataweza kutumia huduma za kusisimua kutoka simu za apps, ambazo huduma na maudhui yake huboresha maisha, kazi na starehe zao. Kuridhika kwa mteja ni kitu cha muhimu sana katika biashara yetu, na ndio maana tunahakikisha kuwa tunabuni huduma na bidhaa zinazoridhisha na kuendana na matakwa ya mteja,” alisema.

Tigo imeanzisha promosheni za kuaminika na zenye uwazi kwa kufanya mawasiliano kuwa sio rahisi tuu kutumia bali zenye thamani.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA