TUME YA KURATIBU MAONI YA KATIBA MPYA YAKABIDHIWA OFISI KATIKA JENGO JIPYA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI

 Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue kushoto akimtembeza Mwenyekiti wa Tume ya kuratibu maoni ya Katiba mpya Waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba  katika ofisi mpya ya Tume hiyo iliyopo katika jengo jipya la Wizara ya mambo ya Ndani ghorofa ya kwanza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika leo kwenye Wizara ya mambo ya ndani jijini Dar es salaam, katikati ni Celina Kombani Waziri wa Sheria na Katiba.
Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue kushoto akimueleza jambo  Mwenyekiti wa Tume ya kuratibu maoni ya Katiba mpya Waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba wakati wa makabidhiano ya  ofisi ya Tume hiyo iliyopo katika jengo jipya la Wizara ya mambo ya Ndani ghorofa ya kwanza , wa pili kutoka kushotoni Celina Kombani Waziri wa Sheria na Katiba na Angela Kairuki mbunge wa CCM viti maalum Dar es salaam
 Ofisi inavyoonekana kwa ndani.
 Mwenyekiti wa Tume ya Kuratibu maoni ya Katiba Mpya Waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Wariomba wa tatu kutoka kulia akiwa pamoja na viongozi wengine wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa hafla hiyo. Chanzo;Full shangwe Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI