UMRI, MAJINA YA LULU YAZUA UTATA MAHAKAMANI

Msanii Elizabeth Michael 'Lulu' ambaye ameshitakiwa kwa tuhuma za kumuua Msanii Nguli nchini, Steven Kanumba akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Magereza alipofikishwa tena leo katika Mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.  

UTATA kuhusu umri wa mtuhumiwa wa kesi ya mauaji, mwigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo umeanza kutoa matokeo, kwenye ya Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam, huku kesi yake ikipigwa tena kalenda hadi Mei 21, mwaka huu.
 
Lulu anayekabiliwa na kesi ya kumuua mwigizaji mwenzake, Steven Charles Kanumba, kwa sasa anasema ana miaka 17, lakini katika mahojiano kwenye kipindi cha TV cha Mikasi, kabla ya kifo cha The Great aliwahi kusema ana umri wa miaka 18.
 
Wakili wa mwigizaji huyo aliyekulia kwenye sanaa hiyo kuanzia akiwa kinda katika kundi la Kaole Sanaa la Magomeni pamoja na marehemu Kanumba, Kenned Fungamtama leo aliwasilisha ombi katika Mahakama hiyo, akiitaka iitupilie mbali kesi hiyo ili ikafunguliwe upya katika Mahakama ya Watoto, akidai Lulu ana umri chini ya miaka 18.
 
Lakini Wakili Mwandamizi wa Serikali, Elizabeth Kaganda alipinga akisema suala hilo, inabidi kwanza lifanyiwe uchunguzi na vyombo vya dola ili kugundua ukweli kuhusu umri wa Lulu(pichani kushoto).
 
Akizungumza mahakamani hapo, Wakili Kaganda alisema mbali na umri wa Lulu kuwa na utata, lakini hata jina lake halisi nalo ni tatizo, pia kwani wakati wengi wanamfahamu kama Elizabeth Michael, lakini cheti chake cha kuzaliwa kinasomeka Diana Elizabeth.
 
Katika ufafanuzi wake, Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando alisema analitupilia mbali ombi la upande wa utetezi, kwa sababu mtuhumiwa anakabiliwa na kesi ya mauji na imefunguliwa chini ya Kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.
Alisema kwa mujibu wa kesi hiyo, Mahakama yake haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo, zaidi ya Mahakama Kuu. Hakimu Mmbando ameiahirisha kesi hiyo hadi Mei 21, mwaka huu.
 
Tayari msisimko wa kesi hiyo unaonekana kuanza kupungua taratibu, kwani leo Lulu aliwasilishwa katika ulinzi wa kawaida na mahakamani hapo hakukuwa na idadi kubwa ya watu, kama ilivyokuwa alipofikishwa mahakamani mara ya pili, mwezi uliopita.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*