Usambazaji umeme wa gesi kukamilika Juni

AWAMU ya pili ya utandazaji wa bomba la umeme wa gesi kutoka Ubungo hadi Mwenge unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Juni mwaka huu 2012.

Hatua hiyo itawezesha nyumba 56 zilizopo eneo la Mikocheni na viwanda sita viliyopo katika eneo hilo kupata huduma ya umeme wa gesi.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi katika mahojiano  jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mtafiti katika Kurugenzi ya Masoko na Uwekezaji wa Shirila la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Emmanuel Gilgert alisema mradi huo pia umetoa matoleo yatakayowezesha pia upatikanaji wa nishati hiyo Chuo cha Maji Rwegarulila.

Maeneo mengine yanayoweza kunufaika ni Sinza, Lugalo Jeshini, Mlimani City na Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), ambapo wakazi wake wataweza kupata umeme wa gesi nyumbani, maofisini na katika migahawa.

Gilbert alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo utategemea upatikanaji wa fedha na kwamba kwa sasa zipo dalili za mipango hiyo kufanikiwa.

Alifafanua kuwa dalili hizo zinatokana na utaratibu wa sasa wa Serikali unaoitaka TPDC kubaki na asilimia 50 ya mauzo ya gesi nchini.

Ofisa huyo alisema kuwa ujenzi wa bomba hilo unazingatia mahitaji ya baadaye, hivyo ukubwa wake pia unaweza kutosheleza mahitaji makubwa ya baadaye kwa wananchi watakaopenda kupata huduma hiyo ya umeme wa uhakika tofauti na ule wa maji, unasambazwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Alisema mradi huo una tofauti na ule wa majaribio ambao unatekelezwa katika nyumba 13 zilizopo katika eneo la nyumba za wafanyakazi wa Mikocheni ambapo gesi inapelekwa kwa magari na kusema kuwa umeme huo ni ghali wakifikiria namna ya kuachana nao.

Mradi huo wa kusambaza gesi unatarajiwa kufuatiwa na mwingine wa bomba kuu la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam utakaosaidia kupunguza utegemezi wa umeme wa Tanesco ambapo utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kutumia zaidi ya Dola za Marekani 55 milioni 55.

Awali, Serikali kupitia wahisani iliweza kutengeneza bomba la gesi kutoka Songo Songo wilayani Mafia hadi Ubungo kwa ajili ya uzalishaji wa umeme ambao unauzwa Tanesco, hata hivyo kutokana na mahitaji kuongezeka bomba hilo sasa limezidiwa na mahitaji.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*