UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU JIJINI MBEYA 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati) akiwasha mwenge wa uhuru kuashiria kuanza kwa mbio za mwenge huo kwa mwaka 2012 leo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. Mwenge huo utakimbizwa kwenye jumla ya Halmashauri za wilaya, Manispaa na miji 157 na kuongozwa na kauli mbiu ya Sensa ya watu na Makazi ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo yetu Shiriki kuhesabiwa Agosti 26.
Waziri Mkuu  Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa vipeperushi vya elimu ya sensa ya watu na makazi itakayofanyika nchini kuanzia Agosti 26 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa mbio za mwenge leo jijini Mbeya. Kushoto ni Kamishna wa Sensa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Hajjat Amina Fatma Mrisho.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara (kushoto) akimtambulisha  kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2012 Kepteni Honest Erenest Mwanossa kutoka Dar es salaam (kulia).
Kiongozi wa mbio za Mwenge Mwaka 2012, Kepteni Honest Erenest  Mwanossa kutoka Dar es salaam akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda tayari kwa kuukabidhi kwa viongozi wa Mkoa wa Mbeya tayari kwa kukimbizwa kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2012, Kepteni Honest Erenest  Mwanossa (kulia) akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro tayari  kwa kukimbizwa kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa huo kabla ya kuelekea mkoani Iringa.
Wananchi na Viongozi mbalimbali wakishuhudia shughuli za kuwashwa kwa Mwenge  wa Uhuru leo jijini Mbeya.
Vijana wa kundi la halaiki kutoka  katika shule mbalimbali za mkoa wa Mbeya wakipamba shughuli za uzinduzi wa mbio za  Mwenge wa Uhuru 2012  zinazoongozwa na kauli mbiu  ya Sensa ya watu na Makazi ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo yetu, Shiriki kuhesabiwa Agosti 26  leo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya .
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakiwa wamevaa T-shirt zenye kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi  2012 leo jijini Mbeya wakati wa uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru.Picha Zote na Aron Msigwa -MAELEZO

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI