Waandishi wa habari Iringa kutumia siku ya uhuru wa vyombo vya habari kwa kumweka kiti moto mbunge Msigwa

Na Francis  Godwin-Iringa

Wakati kesho mei 3 ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ,wanahabari mkoa wa Iringa wamepanga kufanya maandamano makubwa kwa ajili ya kuadhimisha siku hiyo pamoja na kumweka kiti moto mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa baada ya wananchi wengi kumlalamikia mbunge huyo .

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Daud Mwangosi aliyasema hayo leo wakati akizunguza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya siku hiyo ya Uhuru wa Vyombo duniani .

Alisema kuwa mdahalo huu katika ya wapiga kura wa jimbo la Iringa mjini na mbunge huyo wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa utafanyika katika ukumbi wa Highlands ukumbi uliopo katikati ya mji Iringa kutoa nafasi kwa wananchi wote kufika.

Hata hivyo alisema kuwa mdahalo huo ulipangwa kuwahusisha pia wabunge wa CCM akiwemo mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) ambao wameonyesha kuwa na uzuru katika siku hiyo .

Alisema kuwa wakati mbunge Kabati akiomba kutofika kutokana na kuwa katika vikao jijini Dar es Salaam mbunge Filikunjombe kwa siku hiyo atakuwa nje ya nchi hivyo kufika kwao itakuwa vigumu.

Mwangosi alisema sherehe hizo za siku ya uhuru wa vyombo vya habari zitahusisha wanahabari wote bila kujali ni wanachama wa IPC ama si wanachama.

katika hatua nyingine Mwangosi alisema kuwa IPC inasikitishwa na vitendo vitisho vinavyotolewa na wanafunzi wa chuo cha elimu Mkwawa Iringa kwa wanahabari wa vyombo mbali mbali wanaofika kusikiliza madai yao katika migomo mbali mbali.

Alisema kuwa wanafunzi hao wamekuwa na tabia ya kuwaita wanahabari wakati wa migomo yao na mara baada ya kufika na kuripoti wamekuwa wakiwatishia kuwavunjia vifaa vyao vya kazi kwa madai kuwa kwanini wanahabari hao wamewafuata watuhumiwa katika madai hayo na kuwahoji kinyume na wao wanavyotaka kuzungumza wao pekee.

Mwangosi alisema kuwa tayari wanahabari hao wamepata kutoa vitisho kwa mwandishi wa TBC Iringa , Chanel Ten, gazeti la Mtanania ,Habari leo , Radio Ebony Fm ,Radio Country Fm na wanahabari wengine wengi .

Hivyo amesema kuwa iwapo wanafunzi hao wataendelea na tabia hiyo wanahabari hawatakuwa tayari kwenda kuwasikiliza pale wanapohitaji uwepo wa vyombo vya habari katika mambo yao.

Kwa upande wake katibu wa IPC Frank Leonard alisema kuwa mbali ya kumweka mbunge Msigwa pia wanahabari hao watashiriki katika usafi Hospitali ya mkoa wa Iringa pamoja na shughuli nyingine za kijamii mjini Iringa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI