WAFANYA TATHMINI YA MRADI WA SILAHA NDOGONDOGO NA NYEPESI EAC

Na Mwandishi wa EANA
Arusha, Mei 30, 2012 (EANA) – Wakuu wa Vitengo vya Taifa (NFPs) vya Kudhibiti Silaha Ndogondogo na Nyepesi (SALWs) katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameanza Jana kikao cha siku tatu, mjini Nairobi, Kenya, kutathmini matunda yaliyopatikana katika kipindi cha miaka sita cha mradi huo ambao unamalizika mwaka huu.
Mradi huo ulianzishwa kwa juhudi za pamoja kati ya EAC na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kudhibiti uvujaji haramu wa silaha, ambao unasadikiwa kuwa ni chanzo cha uhalifu na uvunjifu wa amani katika nchi za Afrika Mashariki.
Nchi za EAC ni pamoja na Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi.
Pamoja na mambo mengine mradi huo ulikuwa unashughulikia uwekaji alama silaha, kuhamasisha raia juu ya hatari zinazotokana na silaha ndogondogo na kujenga uwezo wa uongozi wa udhibiti silaha (uwekaji alama, usajili na uhifadhi).
Mwenyekiti wa mkutano huo,David Kimaiyo aliziipongeza EAC na GIZ kwa kuanzisha mradi huo muhimu.
“Mradi wa SALWs umekuwa na matokea chanya katika udhibiti wa silaha haramu,’’ Kimaiyo ambaye pia ni Mkurugenzi NFP nchini Kenya alisema katika hotuba yake ya ufunguzi.
Naye Leonard Onyonyi, Mtaalamu wa Amani na Usalama wa EAC, alisema kwamba mkutano huo unalenga kutathmini mafanikio na changamoto za mradi huo wa SALW.
Mkutano huo pia umetoa shukurani za pekee kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa EAC aliyeshughulikia Shirikisho la Siasa, Beatrice Kiraso, kwa mchango wake mkubwa aliokuwa anautoa kwenye mradi huo.
Kiraso aliondoka mwezi uliopita baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa kazi wa miaka sita na EAC.
LC/NI

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*