WASHENZI WACHINJA MTU KAMA KUKU ARUSHA

Na Rose Jackson,Arusha
MTU mmoja aliyetambukika kwa jina Israe Ngonda(45) mkazi wa Kijenge juu jiijini Arusha amekutwa ameuawa kwa kuchinjwa nyumbani.
   Walioshuhudia wamesema baada ya kujinjwa kinyama watu hao wameuacha mwili kitandani ukiwa umepiga magoti na kichwa kulalia kitandani.
   Kwa muijbu wa Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Liberatus Sabas ,mwili wa marehemu ulikutwa asubuhi baada ya majirani kupita eneo hilo na kukuta mlango wa nyumbani kwa marehemu ukiwa wazi ndipo walipojaribu kuingia ndani huku wakimwita jina lake bila  majibu.
    Alisema polisi walipata taarifa na kufika eneo la tukio ambapo walimkuta marehemu huyo akiwa amepiga magoti huku sehemu kubwa ya mwili ukiwa umelazwa kitandani   na sehemu  ya shingo ikiwa imekatwa na kitu chenye ncha kali.
    Aidha Sabas aliongeza kuwa hakuna mtu yoyote anayeshikiliwa hadi sasa kuhusiana na tukio hilo na polisi wameanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
     Taarifa zaidi kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zimedai kuwa kabla ya tukio hilo marehemu alichomewa nyumba yake na watu wasiojulikana na baadae wanakijiji walifanikiwa kuuzima moto huo.
     Imeelezwa kuwa marehemu alikuwa akiishi pekee baada ya familia yake kusafiri na kwamba tukio hilo linahusishwa na ulipizaji wa visasi.
     Tukio kama hilo liliwahi kutokea hivi karibuni wilayani Arumeru, baada ya Mwenyekiti wa Chadema , Kata ya Usariver, Msafiri Mbwambo, kuuawa kwa kuchinjwa na watu wa

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*