Watoto Afrika wanaasiliwa na wageni

Shirika la kuteteta maslahi ya watoto la The African Child Policy Forum linasema zaidi ya watoto elfu 40 wameasiliwa katika kipindi cha miaka minane wengi wakiwa na walezi kutoka Marekani, Ulaya Magharibi na Canada. Watoto wengi hasa wanaasiliwa kutoka Ethiopia ambayo inatuma watoto wengi ugenini nyuma ya China.
Kuna zaidi ya mashirika 70 yanayoshughulika na mpango wa kuwaasili watoto nchini Ethiopia 15 ya mashirika yakiwa ni ya Kimarekani.
Sababu kubwa ya barani Afrika kuwa na idadi kubwa ya watoto wanaoasiliwa na wageni ni kutokana na udhibiti mkubwa wa mpango huu katika mataifa ya Ulaya na Amerika Kusini.
The African Child Policy Forum inasisitiza haja ya kila mtoto kukulia katika mazingira yake asilia ya kuzaliwa. Shirika hili linasema ni muhimu kwa mtoto kukua na jamaa na utamaduni anaofahamu zaidi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.