WATU WANANE HOI KWA KUCHARANGWA NA VISU IRINGA

WATU wanane, wamejeruhiwa vibaya kwa kuchomwa na visu, kabla ya wananchi wenye hasira kali kuteketeza kwa moto, makazi ya kikongwe wa miaka 60 katika Kijiji cha Lupembe, mkoani Njombe.Katika vurugu hizo, Polisi walilazimika kutumia nguvu na kufyatua risasi 16 hewani ili kutawanya wananchi.

Habari za uhakika kutoka katika kijiji hicho na ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, kwa niaba ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Njombe, Fulgence Ngonyani ambaye hajaripoti kazini, zilisema tukio hilo lilitokea juzi usiku.

Wakielezea chanzo cha vurugu hizo, baadhi ya wananchi walisema ni ugomvi wa kulipiza kisasi katika familia ya kikongwe huyo, Rehema Malekela ambaye ni mama mzazi wa Shoto Shabani (38) anayetuhumiwa kuwakata mapanga baadhi ya watu.

Mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo, Tumsifu Kiverege, alisema kabla ya vurugu hizo, mtuhumiwa Shoto alimchoma kisu kichwani, Augustino Msigwa (25) na kumsababishia majeraha.

Inadaiwa kuwa baada ya kumchoma kisu Msigwa, mtuhumiwa aliendelea kufanya hivyo kwa mtu mwingine aliyejitokeza kuamua ugomvi huo jambo ambalo liliwafanya wapige kelele za kuomba msaada na hivyo wananchi kufurika na kuanza kujibu mapigo kwa kumshambulia Shoto.


Hata hivyo polisi waliwahi kufika na kumkamata Shoto ambaye baadaye, alitoroka na kuendeleza vurugu za kuwachoma visu watu, jambo ambalo liliwafanya wananchi kufurika na kuamua kuteketeza kwa moto, nyumba ya mama yake mzazi.

Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, alisema licha ya kuchoma moto nyumba, wananchi pia waliharibu mali mbalimbali za familia ya Rehema na kuvunja vioo vya magari mawili.


Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni Doto Shaban (24), Kulwa Shaban (24), Augustino Msigwa (25), Nashino Kaberege (21) na Angela Hongoli (19) ambaye bado amelezwa katika Hospitali ya Wilaya ya Njombe ya Kibena.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.