WIZARA YA MALIASILI NA UTALII:UWEKEZAJI KWENYE MAENEO YA MALIAKALE UNARUHUSIWA


Wizara ya Maliasili na Utalii imefafanua kuwa kwa mujibu wa Sera ya Malikale ya mwaka 2008 (Kifungu cha 4.5 na 46), wananchi, taasisi mbalimbali, pamoja na wadau wengine wa uhifadhi wanaruhusiwa kumiliki, kulinda, kuhifadhi na kuendeleza urithi wa utamaduni nchini kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho kwa sababu za mafunzo, historia na utalii. Sera pia inaruhusu uwekezaji katika maeneo ya malikale ambao unalenga kuhifadhi na kutumia rasilimali za malikale kama vivutio vya utalii.
Ufafanuzi huu umetolewa kufuatia habari iliyoandikwa na gazeti moja la kila siku kuhusu mwekezaji kumilikishwa isivyo halali eneo lenye magofu ya kihistoria la kisiwa cha Chole kilichopo wilayani Mafia ambayo sasa yanatumika kama sehemu ya hoteli ya kitalii.
Wizara kupitia Idara ya Mambo ya Kale inatambua kuwa magofu ya kihistoria katika kisiwa cha Chole ni Kumbukumbu za Urithi wa Utamaduni yenye umuhimu kitaifa na kimataifa na Magofu haya yanalindwa na Sheria ya Mambo ya Kale Na. 10 ya mwaka 1964 na marekebisho yake Na 22 ya mwaka 1979. Idara inawajibika kusimamia uhifadhi na uendelelezaji wake kulingana na kanuni na miongozo ya uhifadhi na uendelelezaji.
Wizara inasisitiza kuwa siyo maeneo yote ya urithi wa utamaduni yanasimamiwa na Idara ya Mambo ya Kale moja kwa moja. Maeneo ya urithi wa utamaduni yenye sifa za kitaifa ni mengi lakini 12 tu ndiyo yanayomilikiwa na Serikali Kuu na kuendelezwa na Idara ya Mambo ya Kale. Maeneo yaliyo mengi yanamilikiwa na watu binafsi, taasisi za umma na binafsi na vijiji au wilaya. Kwa mfano, Magofu ya Chole, Mafia hayapo chini ya umiliki wa Idara ya Mambo ya Kale moja kwa moja bali yapo chini ya umiliki wa wilaya na serikali ya kijiji cha Chole.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.